Jeff Gemo
Member
- Jul 11, 2015
- 34
- 26
Tasnia ya soka la bongo limegubikwa na mambo mengi ya ajabu, wenye taaluma hawapewi nafasi ya kuongoza, wenye nafasi hawataki taaluma ya kuongoza. Ukiwauliza unaambiwa "uongozi ni karama"
Uchezaji mpira ni kipaji, unaongezea mazoezi na kujituma unakuwa mchezaji bora, sina ubishi na hilo wala sitabisha ukisema vinginevyo.
Shida kubwa ni Uongozi wa mpira!
Watu wengi walio katika mfumo huu hawana taaluma na tasnia na mbaya zaidi hata passion tu ya kutaka kujua "do's & dont's" hawana. Na ndio maana maamuzi na mipango mingi ya soka la Tanzania huwa ni zengwe na kitendawili.
Lakini jambo lingine ni kwetu wadau wa soka, huwa tunaona kiongozi bora ni yule anayesikikiza unachotaka hata kama hakiko sahihi. Tunakwenda kwa mihemko na kuamua kwa mikurupuko, tunakosa mashiko na kuendekeza ujiko.
Kiongozi bora ni yule anayeweza kukusaidia kufikiri kwa usahihi (kwa kuwa ni mwanataaluma na wewe sio), anaweza kusimamia maamuzi sahihi ya wakati ujao hata kama sio sahihi kwa wakati uliopo, anaweza kutumia utashi kupata masuluhisho sahihi ya migogoro hata kama atapingwa na watu wote, the truth shall set him/her free.
Taasisi za mpira wa Tanzania zinaongozwa kulingana na presha za watu, sio presha za maendeleo ya nyanja hii. Kuna maeneo yananuka rushwa na uozo wa hongo, kuna kutu ya ubinafsi na madoa ya majungu, vinapasua na kutenganisha wapenzi wao.
Chaguzi zikifika ni wakati wa wapiga kura kunufaika, ni muda ambao TAKUKURU inasahaulika na hakuna anayejali, ukiingia madarakani kwa hongo au rushwa, basi kipindi chote cha uongozi wako utatafunwa na dhambi hiyo, na ukitumika na ukakubali kuwekwa madarakani basi kipindi chote cha uongozi utamtumikia na kusikiliza aliyekuweka.
Mwisho wa siku ikumbukwe uongozi ni dhamana, ipo siku mtu atakaa katika nafasi yako na kufanya mambo makubwa, kila mtu atakudharau na wenye hasira watakupiga mawe.
Jeff Gemo Mnyama Machine
The One Man Army
Affirmative Gemo The Great
[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Season 2 | Episode One.