Nasubiri kuona mpambana. Kitumbua cha 22 years SSH kawaondoa.Ila jamaa kwa nini wasingeboresha tu? A good businessman knows how to make it workKama Serikali ni Safi hakuna haja ya kuogopa kuchafuliwa
Wazee miaka 22 walikaa pale nahisi walishajua hadi wanakufa bila kutoka mama kaja kapita na kichwa asubuhi mapemaAcha wafu wauane wenywe..
Haya mambo yanahiyaji dua piaTanzania kwanza mengine baadae
Ngoja tuone!!Kuna tetesi zinaenea kuwa kampuni ya kimataifa ya kuhudumia makontena (TICTS) imeanza operesheni maalumu ya kuichafua serikali ya Tanzania ndani ya nje ya Tanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Hatua hii ya TICTS inatokana na serikali kuamua kuvunja mkataba wa TICTS na Serikali kuhudumia makontena kwenda bandari ya Dar. Serikali imesema mkataba huo uliodumu kwa miaka 22 umevunjwa baada ya TICTS kushindwa kufanya marekebisho ya kiutendaji waliyokuwa wakipewa na serikali kuanzia mwaka 2013.
Serikali imesema kushindwa kwa TICTS kufanya kazi kwa ufanisi kumechangia Tanzania kurudi nyuma kibiashara ukilinganisha na bandari nyingine za nchi jirani kama Mombasa Kenya. Imeongeza kuwa mkataba huo umevunjwa kunusuru bandari, uchumi wa Tanzania na ajira za wananchi wanaotegemea bandari.
Hata hivyo vyanzo vya ndani vinaeleza TICTS wamepokea uamuzi huo kwa shingo upande na wameapa kupambana na serikali. TICTS ina wabia wawili wakubwa Tanzania mmoja ni Nazir Karamagi (Waziri wa zamani mwenye kashfa ya kuwahi kusaini mikataba ya madini ya migodi ya Tanzania hotelini nchini Uingereza) na Yogesh Manek (mfanyabiashara mwenye benki ya Exim Tanzania). Wawili hao wana ubia na kampuni ya Hutchison Port Holdings Limited ya Hong Kong.
Chanzo cha habari kimeonesha orodha ya vyombo 9 vya habari Tanzania ambavyo TICTS wanajaribu kuvinunua katika kazi hiyo ikiwemo gazeti la Mwananchi. Shauku ya wadau wengi ni kuona namna gani TICTS wataweza kuishinda serikali katika vita hiyo waliyoamua kuitangaza.
Ni kweli kabisa hii ni nchi yetu hatuna pa kwenda lazima tuilinde nchi yetu kwa ghalama Mungu hawezi tuacha .Haya mambo yanahiyaji dua pia
Kuna tetesi zinaenea kuwa kampuni ya kimataifa ya kuhudumia makontena (TICTS) imeanza operesheni maalumu ya kuichafua serikali ya Tanzania ndani ya nje ya Tanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Hatua hii ya TICTS inatokana na serikali kuamua kuvunja mkataba wa TICTS na Serikali kuhudumia makontena kwenda bandari ya Dar. Serikali imesema mkataba huo uliodumu kwa miaka 22 umevunjwa baada ya TICTS kushindwa kufanya marekebisho ya kiutendaji waliyokuwa wakipewa na serikali kuanzia mwaka 2013.
Serikali imesema kushindwa kwa TICTS kufanya kazi kwa ufanisi kumechangia Tanzania kurudi nyuma kibiashara ukilinganisha na bandari nyingine za nchi jirani kama Mombasa Kenya. Imeongeza kuwa mkataba huo umevunjwa kunusuru bandari, uchumi wa Tanzania na ajira za wananchi wanaotegemea bandari.
Hata hivyo vyanzo vya ndani vinaeleza TICTS wamepokea uamuzi huo kwa shingo upande na wameapa kupambana na serikali. TICTS ina wabia wawili wakubwa Tanzania mmoja ni Nazir Karamagi (Waziri wa zamani mwenye kashfa ya kuwahi kusaini mikataba ya madini ya migodi ya Tanzania hotelini nchini Uingereza) na Yogesh Manek (mfanyabiashara mwenye benki ya Exim Tanzania). Wawili hao wana ubia na kampuni ya Hutchison Port Holdings Limited ya Hong Kong.
Chanzo cha habari kimeonesha orodha ya vyombo 9 vya habari Tanzania ambavyo TICTS wanajaribu kuvinunua katika kazi hiyo ikiwemo gazeti la Mwananchi. Shauku ya wadau wengi ni kuona namna gani TICTS wataweza kuishinda serikali katika vita hiyo waliyoamua kuitangaza.
Utakuta kilichofanyika ni kuwanyang'anya kina Karamagi na kuwapa kina GSM ambao ndio msoga line [emoji23][emoji23][emoji23]!!!
Tegemeeni kupigwa wharfage na storage fees kama kazi hivi. Maumivu yatakuwa XXL hadi hao TICTS mtawakumbuka.
KARAMAGI kesha kuwa Mwenyekiti wa CCM MKOA hakuna SHIDA Atarudishiwa KAMPUNI YAKE Ukiwa CCM Hakuna kinachoshindikana CCM inaweza Kumzuia hata Mwanachama wake KUFAKaramagi wa TICTS' ahaha kwa wahariri, wabunge
* Ni baada ya mkataba wao kufutwa bandari ya Dar es Salaam
* Kampuni ya PR ya Capital Plus yapewa kazi kuisafisha TICTS
* Wapanga uhujumu wa huduma za makontena bandarini baada ya kuenguliwa
WAZIRI mstaafu Nazir Karamagi na mfanyabiashara Yogesh Manek wameanza kampeni mahsusi kwa wahariri na wabunge kujaribu kuikwamua kampuni yao ya TICTS ambayo imefutiwa mkataba wa kuendesha eneo la makontena kwenye bandari ya Dar es Salaam.
TICTS wamefutiwa mkataba huo baada ya kushindwa kuonesha ufanisi kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
"Karamagi na Yogesh wanahaha kila kona kujaribu kushawishi wahariri, wabunge na maafisa waandamizi wa serikali wairejeshee mkataba huo," alisema mfanyakazi mmoja wa kampuni ya uchukuzi.
"Wanataka kuwaweka sawa wahariri ili waanze kampeni kwenye vyombo vya habari ya kuitetea TICTS irejeshewe mkataba"
Taarifa zinasema kuwa TICTS wameajiri kampuni ya PR ya Capital Plus kufanya kazi ya kuwasafisha kwenye vyombo vya habari."
Vyanzo vyetu vya habari vinasema kuwa baadhi ya watumishi wa TICTS wanapanga kufanya hujuma kwenye huduma za makontena bandari ya Dar es Salaam baada ya mkataba wao kwa hasira ya kusitishiwa mkataba.
"Huenda tukasikia huduma za makontena bandari ya Dar es Salaam zimesimama ghafla kwa hujuma baada ya TICTS kufutiwa mkataba kabla mwekezaji mpya hajaja," alisema.
Mkataba umevunjwa au ume expire? Naomba ufafanuzi kwa anayejua.Karamagi wa TICTS' ahaha kwa wahariri, wabunge