Karata 3 za Shin Se Kyung wa 6 Flying Dragons

Karata 3 za Shin Se Kyung wa 6 Flying Dragons

Tea Party

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2019
Posts
658
Reaction score
1,133
Kabla sijafuatilia historia yake sikuwahi kujua kama anatimiza miaka 31 mwaka huu.. Anaonekana ni mdogo, ni kama hakui hivi.

Shin Se Kyung ndio jina lake na of course ameigiza series nyingi sana, binafsi nilianza kumuona kwenye FASHION KING (2012), THE GIRL WHO SEES SMELL (2015) na yangu pendwa kabisa SIX FLYING DRAGONS (2015)

Leo tarehe 21 May 2021 naomba nilete kwa haraka haraka mambo matatu usiyoyafahamu kuhusu mwanadada huyu aliyezaliwa 1990.

3. Se Kyung ni msomi na uigizaji ndio kitu alichosomea. Ukweli usemwe dada huyu ana degree ya Perfoming Arts kutoka kwenye Chuo Kikuu cha Chung Ang University, chuo ambacho wasanii au tuseme waigizaji wengine kama GO ARA, HYUN BIN, CHOI TAE HYUN na JANG NARA wamesoma.

Tunachokipata hapa ni kwamba pamoja na kipaji alichonacho Shin aliamua kuingia darasani kuongeza ujuzi. Nadhani hii ndo imemfanya awe na uwezo na kucheza characters nyingi nyingi.

Namna ambavyo alicheza Fashion King ni tofauti kabisa alivyocheza kwenye Six flying dragons yaani ni kipaji haswaa kilichojazwa na elimu.

2. Shin ameanza kuigiza tangu akiwa na miaka nane (8). Historia inasema mwanamuziki Seo Taiji ndiye aliyemtambulisha Shin kwenye Kiwanja cha burudani mwaka 2008 baada ya Shin kutokea kwenye album cover ya msanii huyo.

Baada ya hapo Shin akaanza kuitwa kwenye vipindi tofauti tofauti vya watoto. Kitanzania tungeweza kumfananisha na Lulu kipindi kile ni mtangazaji wa kipindi cha WATOTO WETU pale ITV.

Shin alikuwa ni mtangazaji wa kipindi cha watoto cha Ppo Ppo Ppo na hapo ndipo akapata umaaruf zaidi na alipokuwa na miaka 14 tu akapata nafasi kwenye series ya MY LITTLE BRIDE (2004) huku 2006 akapata nafasi kwrnye series ya CINDERELLA.

1) Kuna kipindi nadhani ni 2010 Shin alikuwa kwenye mahusiano na Kim Jong hyun. Kim Jong hyun alikuwa ni mmoja ya wanamuziki wa kundi la Shinee.

Baada ya muda kidogo waliachana lakini kikubwa ni kuwa ilipofika 2017 Kim Jong hyun alijiua baada ya kupata msongo wa mawazo (Depression).

Wanasema kuachana sio uadui maana Shin alikuwepo kwenye siku ya msiba wa Jong Hyun tena alikesha kabisa na alisikitika sana maana hata baada ya kuachana walibaki kuwa marafiki wazuri tu.

Okay hizo ndio Karata Tatu kwa leo. Vipi una kingine unakifahamu kuhusu Shin Se Kyung. Usiache kutoa maoni yako.


Shin_Se-Kyung-p3.jpg
shin-se-kyung-3.jpg
_ssk2.jpg
20101027_ssk_jonghyun_4.jpg
 
Back
Top Bottom