Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Baada ya mbinu chafu za CCM kujulikana za kuwaandaa wapigakura kuyapokea matokeo yaliyo batili katika uchaguzi mkuu kwa kupitia vyombo vilivyokithiri kwa ufisadi vya REDET na SYNOVATE yenye kulenga kuonyesha upinzani bado ni dhaifu Tanzania wakati sivyo hivyo hata kidogo, ushauri wangu kwa Chadema ni kucheza karata turufu itakayolinda na kuheshimu matakwa ya watanzania walio wengi ambayo ni hii hapa:-
a) Kuishinikiza NEC kuwarudishia wapigakura haki yao ya kimsingi ya kulinda kura zao ili zisije kuchakachuliwa kwa kurudisha utaratibu wa wapigakura kuwa mita 200 kutoka vituo vyao walivyopigia kura.
Lengo ni kuwazuia mashushushu waliotapakazwa nchi nzima kuja kuchakachua matokeo kwenye vituo vya kuhesabia kura kwa kuwarubuni mawakala wao kwa maburungutu ya fedha.
b) Kuwalipa mawakala wao wote badala ya kuwaachia zigo hilo wagombea ambao wengi wao ni hoehae.
Gharama za kuwalipa mawakala wote ambao hufikia takribani ya watu 53, 000 kwa siku moja kwa shilingi 12, 000/= kila mtu, Chadema itatumia jumla ya Tshs 1.06 bilioni shilingi.
BIla ya kufanya haya mawili Chadema itakuwa imetusaliti sisi wapigakura ambao tuna imani nao kuwa ni wakombozi wa Nchi hii kutoka minyororo ya utumwa wa CCM.
Mabadiliko ya utawala yanahitaji wote tujitume lakini Chadema isitarajie wapigakura tutajituma zaidi ya kupiga kura kama hawatatuwezesha kuwasaidia kulinda kura.
Kamwe hatuwezi kulinda kura kutoka majumbani ambako ndiko NEC inatuagiza twende kujisitiri wakati wao NEC na CCM wanatufanyizia mambo yao machafu machoni pa Mwenyezi Mungu...................DHULUMA