Mimi nafikiri tofauti kidogo kuhusu suala la Karia. Karia arudi au asirudi TFF sio suala kubwa. Suala kubwa kwenye uchaguzi wa TFF ni ile kanuni ya hovyo kabisa ya udhamini wa wajumbe watano kwa wagombea uraisi na sijui wajumbe waliipitisha wakiwa wamelala au vipi. Haiwezekani watu waliochukua fomu wakienda kila mkoa kuomba udhamini wanaambiwa eti wameshamdhamini Karia. Maana yake hali ikiendelea hivi Karia atapita bila kupingwa hivyo uchaguzi utakuwa sio huru wala wa haki. Tunajua Karia alikuwa madarakani muda mrefu na amewashika wajumbe wengi mikoani lakini kwa nini atumie mbinu za hovyo kiasi hicho kurudi madarakani. Kama amefanya mazuri na wajumbe wanamkubali kwa nini ahofie kiasi cha kutumia mbinu chafu za namna hiyo? Si wajumbe kama wanamkubali watamrudisha kwa kishindo kwenye sanduku la kura.
Mbaya zaidi sisi watanzania hatusomi vitu vya muhimu kama katiba. Eti mtu anaenda kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa TTF na huku hajui kuna kipengele cha hovyo kinachombeba Karia halafu akishakwama huko anarudi kulalamika kwenye vyombo vya habari kuhusu hicho kifungu baada ya kukwama kupata wajumbe watano watakaomdhamini. Mimi nafikiri ni wakati sasa wa wagombea aidha kwenda kwa msajili wa vyama au ikiwezekana waende mahakamani kabisa kukipinga hicho kifungu na ikiwezekane uchaguzi uhairishwe mpaka hicho kifungu kiondoke. Na hata mbinu nyingine chafuna za hovyo za kuwaondoa watu "potential" kama Ali Mayay zisipewe nafasi kabisa jkatika uchguzi huo wa TFF.
Kinachotakiwa ni uchaguzi huru na wa haki bila figisu figisu. Ashinde Karia au yoyote yule si suala kubwa sasa bali haki itendeke na ionekane kweli imetendeka kwa wagombea wote.