Karia na TFF wasipowafanyia fitna Kambole na Djuma Shaban itakuwa balaa sana

Karia na TFF wasipowafanyia fitna Kambole na Djuma Shaban itakuwa balaa sana

njaakalihatari

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2019
Posts
4,081
Reaction score
8,671
Sisi sote ni mashahidi jinsi wallace karia na TFF walivyokuwa wanawazuia kina yikpe,sarpong na wachezaji kadhaa nyota wa kigeni kufunga magoali na kusababisha wakose magoli ya wazi huku wakiwabeba wachezaji wa kiwango cha kawaida mno kama cham,kagere,luis jose waonekane wana shine.

Wana jangwani tumechoka na fitna hizo, haiwezekani wachambuzi na manguli ya habari kama gazeti la mwana spoti wachambue na kusema mashine/mitambo ya magoli inashuka ikifika hapa TFF wanafanya fitna, mitambo inaonekana ya kawaida, siyo uungwana huu.

Kambole na Djuma Shabani ambao kwa pamoja wameigharimu Gsm ths billions 6.2 wasipozuiwa na Karia ku shine uwanjani watatisha sana na kama wasipofanya vizuri lawama ziende TFF.
 
Mtambo wa magoli umeingia dar. Umepewa faili la wawa na onyango.

Nikikumbuka hii natabasamu tu mwenyewe. Yanga timu yangu ina raha sana. Hata kama hujapata ushindi.. unapata sababu ya kucheka kwa vituko
 
[emoji16][emoji16][emoji16]sema sisi Yanga kwa kulalamika?
 
Akili za Utopolo bhana,hayo yote mmeyasema sana miaka ya nyuma lakini mwisho wa siku mnaanza lawama,mnaenda uwaja wa ndege mkimanisha wasahabiki wenu kuwa mnaleta wachezaji wa maana kumba magalasa tu,sasa hivi mmeanza na mbwembwe zenu zile zile lakini muda huwa ni Mwl mzuri.
 
Lawama atapewa msolla wakati injinia anasajiri mida hii kaweka kambi Congo kujizolea wachezaji wa bure
IMG-20210614-WA0025.jpg
 
Mtoa mada umeongea POINTI TUPU. Maana wachezaji mitambo ya magoli wakitua tu upande wa sisi utopolo, Kaia anawaita na kuwatisha endapo wakifunga atawafukuza nchini warudi walikotoka bila visa. SISI WATOPOLO TUMEONEWA MIAKA YOTE MI4 YA KARIA NA TFF YAKE.
 
Akili za Utopolo bhana,hayo yote mmeyasema sana miaka ya nyuma lakini mwisho wa siku mnaanza lawama,mnaenda uwaja wa ndege mkimanisha wasahabiki wenu kuwa mnaleta wachezaji wa maana kumba magalasa tu,sasa hivi mmeanza na mbwembwe zenu zile zile lakini muda huwa ni Mwl mzuri.
Mbona huu uzi kama wa kukejeli Fulani?.
 
Mtoa mada umeongea POINTI TUPU. Maana wachezaji mitambo ya magoli wakitua tu upande wa sisi utopolo, Kaia anawaita na kuwatisha endapo wakifunga atawafukuza nchini warudi walikotoka bila visa. SISI WATOPOLO TUMEONEWA MIAKA YOTE MI4 YA KARIA NA TFF YAKE.
Hahahaha!! Nyie watopolo siyo?.
 
Back
Top Bottom