Drat
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 1,160
- 1,359
Mchezo huu ambao huteka hisia za mashabiki wengi wa mpira wa miguu, utakuwa na msisimko mkubwa sana.
Sababu ikiwa ni kila timu kuwa wakati wa kipekee, Yanga akiwa kabeba ubingwa bila kupoteza mechi lakini kashindwa kwenda hatua ya makundi, anasubiri kucheza na Africain ili afanikishe kwenda makundi shirikisho.
Ikiwa ni Yanga iliyokuwa na matumaini makubwa kwa miaka ya karibuni baada ya kufanya usajili mzuri chini ya mwekezaji GSM.
Simba ikiwa imepoteza mataji yote, kuachana na nyota wake kadhaa kama Mugalu, Kagere, Wawa, na Dejan. Pia kuachana na kocha wa kigeni na kuwa chini ya kocha Juma Mgunda ambae haijulikani kama bado ni kocha wa mpito au kashafika.
Lakini Simba wakifanikiwa kwenda hatua ya makundi Klabu Bingwa Afrika.
***********
Katika uwanja mtazamo wangu ni kuwa, utakuwa mchezo wa mbinu na akili nyingi.
Yanga Kushinda
Yanga atashinda endapo ataiheshimu Simba na kucheza kwa tahadhari na kukaba kuanzia katikati, ili wawahi kujaa nyuma endapo Simba atafanikiwa kuvuka eneo la nusu ya pili ya Yanga.
Pia itawasaidia kuhimili mashambulizi ya kujibu ya Simba, ambao wamekuwa wazuri katika hilo na Yanga kama tulivyoona katika mechi yao na Al Hilal wamekuwa wazembe sana katika hilo.
Simba Kushinda
Simba watashinda endapo watadhibiti eneo la katikati kwa wakati wakitumia nguvu kubwa, matumizi ya krosi za chini, na krosi za juu za lakini mipira idondokee nje ya eneo la hatua sita la goli kipa.
Sare
Matokeo ya sare kwa mtazamo wangu binafsi, nafasi yake ni ndogo. Kila timu inahitaji nafasi hii ili ishike usakani wa kuongoza ligi.
Matokeo baada ya mechi
Simba: Mgunda ataaminiwa zaidi, morali ya timu Klabu Bingwa itaongezeka endapo ikishinda. Kinyume na hapo suala la kocha litaanza kuongelewa upya, wachezaji watapata wakati mgumu kisaikolojia hasa kutoka kwa mashabiki.
Yanga: Nabi atarejesha furaha na kusahau yaliyopita kwa muda, na itaongeza hamasa na tumaini la kushinda mechi ya kufuzu hatua ya makundi shirikisho. Endapo Yanga itafungwa, kondoo wa sadaka atatafutwa, ni mechi ngumu kwa kocha na usajili mpya (Aziz Ki, Morisson, Bigirimana) ikileta matokeo mabaya, Lomalisa wataonekana hawana msaada.
Kila la heri. Kwa maslahi yangu binafsi Simba ishinde, mimi ni shabiki wa Simba.
Shukrani, Mtaaaniiii tarehe ishirini na tatuuuu.