Nokla
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 3,190
- 1,774
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeupangia tarehe mchezo namba 180 wa Ligi Kuu msimu wa 2023/2024 kati ya Club ya Yanga na Club ya Simba maarufu kama ‘Kariakoo Derby’, baada ya Club hizo kuondolewa kwenye michuano ya CAF Champions League.
“Mchezo huo ambao haukupangiwa tarehe kwenye ratiba iliyofanyiwa maboresho na kutangazwa February 2024, sasa utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa April 20, 2024 kuanzia saa 11:00 jioni na tayari Club za Yanga na Simba pamoja na Wadau wengine wa Ligi Kuu wamepatiwa taarifa zote kuhusiana na mchezo huo na maandalizi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mikubwa ya Ligi ya sita kwa ubora Barani Afrika”