Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Licha ya kutambulika wazi kwamba Kariakoo ni sehemu muhimu ya kibiashara ambayo inajumuisha shughuli mbalimbali ambazo zinafanya kuwa chanzo nyeti cha mapato nchini, lakini nashangazwa na mamlaka kushindwa kuwajibika kuzingatia usafi wa mazingira katika eneo hilo.
Ni zaidi ya Wiki mbili sasa kuna chemba zinatema maji machafu na taka, jambo la kusikitisha chemba hizo zinatililisha uchafu huo kwenye maeneo ambayo watu wanapita pamoaja na magari.
Lakini kibaya zaidi unakuta pembeni mwa barabara watu wamepanga bidhaa za chakula huku maji ya machafu yanayotimuliwa na magari yakidondokea vitu hivyo, jambo ambalo ni hatari kwa walaji, mfano eneo la njia panda karibia na Soko(Mtaa wa Pemba) na Mtaa na Mtaa wa Nyamwezi ambako Watu wanapanga chini matunda na viungo vya vyakula.
Soma Pia: Kituo cha Mwendokasi Kimara acheni kutiririsha maji machafu usiku
Hali hiyo sio rafiki na imekuwa endelevu kwa kujitokeza mara kwa mara, siwezi kukaa kimya kwa sababu tunao Viongozi wa Jiji ambao wanatakiwa kusimamia mambo kama hayo, najiuliza viongozi wetu hao kama wameweza kuweka Watu wa kukusanya ushuru kila siku, iweje sasa wakose taarifa za chemba kuhatarisha afya za Watu.
Kushindwa kuweka eneo la Kariakoo katika mazingira salama ni sawa na kutuma meseji kwa Watu kwamba wasije eneo hilo au waje kwa tahadhari zaidi.