Kariakoo kuvutia wateja wa nchi tisa Dar es Salaam kupitia Kariakoo Festival

Kariakoo kuvutia wateja wa nchi tisa Dar es Salaam kupitia Kariakoo Festival

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
17 JULY 2024

Kariakoo Festival PNG Logo


MSIMU WA PUNGUZO​

#Twenzetu​

Kariakoo​

Kariakoo Festival 2024 inakuunganisha na Biahara zinazo toa Punguzo la bei katika msimu huu.

KARIAKOO KUVUTIA WATEJA WA NCHI TISA DAR ES SALAAM KUPITIA KARIAKOO FESTIVAL


View: https://m.youtube.com/watch?v=CD3i4rnF-h4&pp=ygURS0FSSUFLT08gRkVTVElWQUw%3D

KARIAKOO FESTIVAL KUWAUNGANISHA WAFANYABIASHARA ZAIDI YA ELFU THELATHINI NA TANO

wafanyabiashara, TRA soko la sale sale kwa nchi 8 zinazoizunguka Tanzania na wateja wa ndani.

lengo ni kuifunguka Kariakoo mpya kupitia Kariakoo Festival ili kuitangaza na kubadilisha fikra za wanunuzi, TRA, watu wa cargo ili kuitangaza na kuvutia wateja kutoka eneo hili la Afrika ya Mashariki, Maziwa Makuu na Kusini mwa Afrika
 
Jinsi kampuni ya TEMU Online ya China inavyounganisha wadau wafanyabiashara 100,000 kufanya biashara na ulimwengu.


View: https://m.youtube.com/watch?v=ZvC_QLrBfUM

Nchi zifuatazo haziangaiki ku declare ili kukagua vifurishi vya bidhaa kutoka nje vilivyo na thamani zifuatazo :
  • Marekani mzigo wa US$ 800 haukaguliwi kulipia kodi
  • Umoja wa Ulaya bidhaa kadhaa ya Euro 150
  • Japani 100,000 Japan Yen
  • Uingereza 135 Pound sterlings
  • China 50 Yuan China
  • Canada 20 Canadian Dollars
Je Kariakoo na Mamlaka ya Mapato Tanzania imejipanga vipi vifurushi viendavyo kwenye nchi 9 zinazoizunguka Tanzania kutotozwa kodi kwa bidhaa kwa kiwango fulani, au kila kitu kitakuwa kinafukuziwa na task force ya TRA kukusanya kodi kwa kutumia hela nyingi za operesheni kukusanya kodi hivyo Kariakoo kushindwa kuwa kitovu cha biashara eneo hili la Afrika kama ilivyo katika ndoto kupitia Kariakoo Festival ?

Inasikitisha mtanzania akitaka kusafirisha kifurushi cha bidhaa mchanganyiko hata cha thamani chini ya Tshs. 500,000 atatozwa kodi kubwa na posta, DHL, TRA n.k hivyo kuifanya nchi kushindwa kufunguka kibiashara kama ambavyo awamu ya sita ya Dr. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyohubiri kuifungua nchi.

Ndiyo maana kampuni kama AMAZON, TEMU, ALIBABA n.k zinatumia fursa hizi kujipenyeza katika nchi mbalimbali ambazo hazifuatili mzigo wa bidhaa mchanganyiko chini ya kiasi fulani kama ilivyobainishwa hapo juu.

Na faida zake mtambuka ni kubwa, hivyo TRA wizara ya fedha, wizara ya viwanda Tanzania wajipange kutumia fursa hii ya Tanzania kuwepo ktk eneo la kijiografia ifaidike kuongeza ajiri, fedha za kigeni n.k
 
Back
Top Bottom