crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,193
- 810
Kariakoo ni fursa kubwa ya kiuchumu kwa Tanzania. Soko hili linazihudumia nchi jirani za EA na za kanda ya kusini kam Congo, Zambia, Rwanda, Malawi, Zimbabwe n.k
Kama tungekuwa tunaliona hili kwa mtazam8 mpana, soko la Kariakoo lisingekuwa linaendeshwa kama gulio tu. Matokeo ya uendeshaji na mipango mibovu, utafiti mdogo unaonyesha watu wengi hawapendi kwenda Kariakoo sababu ya msongamano, kutokuwepo parking, vibaka na matapeli, mipangilio mibovu ya maduka inayomfabya mtu kuzunguka weee kutafuta bidhaa.
Ili kukabiliana na hayo, maboresho na mageuzi makubwa ya uendeshaji yanahitajika ili ku tap hiyo business potential tuliyokuwa nao. Natoa mchango wangu hapa
1. Magari, bajaji na maguta yazuiwe kupaki eneo la maduka kusubiri wateja. WATENGEWE ENEO lao kama Jangwani, mfumo kama uber, unaweza kutumika ili wakija wanapakia na kuondoka. Hii itapunguza sana msongamano.
2. Ruti ya Fery_Kariakoo ya Bajaj ifutwe. Utumike mwendokasi tu, maana nazo zina fujo na kuongeza msongamano.
3. Biashara kandokando ya barabara au barabarani au vibarazani zifutwe na iwe ni takwa la kisera sio huruma za wanasiasa.
4. Kuwe na mpangilio wa maduka ili yanayotoa huduma ya aina moja yakae sehemu moja. Hii itarahisisha movement
5. Ziwekwe sehemu za kupumzika sehembu mbalimbali ili kufanya shopping iwe enjoyable.
6. Uimarishwe usafi
7. Baadhi ya naduka yatoe huduma hadi angalau saa 4 usiku ili kuongeza flexibility. Mfano watumishi wanaweza jutoka kazini wakafanya shopping badala ya watu wote kurundikana masaa yaleyale, na hii siyo kukurupuka tu sababu ya sikukuu.