Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Wafanyabishara wanauliza Mmachinga ni nani ?
Je watu kama hawa mwenye vyombo vingi kiwango hiki ,wanapanga barabarani vyombo vyote hivi bado wanasifa za kuitwa Wamachinga. Mtu ambaye ana bidhaa ukizijaza kwenye duka moja havitoshei eti ni machinga lakini bidhaa hizo hizo nje ya kariakoo ukiziweka kwenye fremu ya elfu thelathini unalipishwa lodi zote na EFD unalazimishwa uwe nayo !pathetic
Hizo Carpet hapa Singida ni duka kubwa tena katikati ya mji, eti kwa Dar wanaitwa machinga, WTF!
Machunga anapaswa asizidishe kapeti mbili !
Bado kwa mtaji mkubwa wa watu hawa ,wanapaswa bado kuitwa Wamachinga..?
Watu hawa;____
1.Hawalipi kodi ya pango.
2.Hawadaiwi risiti na hawatoi risiti
3.Hawalipi kodi ya TRA.
4.Hawasumbuliwi na Halmashauri ya Jiji wala TRA Kipata.
5.Wanapanga biashara zao katikati ya barabara.
6.Wanazuia biashara za maduka ya wenzao wanaolipa kodi TRA zisionekane vizuri.
7.Wanazuia Wateja kupita katika maduka ya wenzao wanaolipa kodi TRA.
8.Wanazuia wenye maduka na store wanaolipa kodi TRA wasipitishe mizigo yao.
9.Wenzao wakilalamikia utitiri wa kodi wao wanachekelea ,kwa sababu hawalipi kodi ya aina yoyote.
10.Serikali haiwasumbui,haiwaondoi,haiwaoni,haina habari nao.
NINI HAKIFANYIKI:
1. Machinga wanatumiwa kama wapigakura na wanatumiwa kisiasa, inafahamika kabisa kama wangelipa
kodi serikali isingekopa korea wala China wala dubai.
2. Wanatumiwa kuuza magendo yanayoibwa yard na pia kuuza bidhaa feki, zilizo expire na zilizotolewa
kwaajili ya kuteketezwa Pugu wao wanaziingiza tena.
3. Wanatumiwa na wenye maduka kukwepa kodi, mwenye duka awagawai machinga bidhaa alafu ana under
declare mapato TRA na hivyo kuepuka kodi[evasion]
NINI KIFANYIKE:
1. Ondoa machinga wote.
2. Barabara zote za kariakoo zipitike.
3. Fungua soko la Machinga complex , watu wauzie ndani.
4 .BRELA ihakikishe wamachinga wote wansajili biashatra zao, manispaa wahkikishe wafanya
biashara wote wanachukua leseni na mikataba yote ya pango ilipiwe ushuru wa stempu.
5. wamachinga nao watoe EFD kama wenye maduka.
AMBOCHO HAKITOKAA KIFANYIKE MPAKA KIYAMA:
1. Wamachinga hawatokaa kuondolewa barabarani maana ni mtaji wa kura za CHAMA TAWALA.
2. Wamachinga hawatakaa watoe risiti maana wanajifanya hawawezi kununua EFD.
3. Soko litaendelea kuwa holela na kichaka cha ukwepaji kodi mkubwa!
4. Wamachinga wataaminishwa wao ni maskini na wenye maduka wao ni matairi hivyo tabaka kutengenezwa na machinga kuendelea kubakisha madarakani chama kilichopo.
LA KUJIFUNZA:
Maandamano ya Gen-Z hapo kenya ni funzo kwa watawala, kwa yule liwali wa Dar anayehisi ni "mungu mtu" !
NOTA BENE: Wafanyabiashara kariakoo hawana matatizo na wanachinga wanaotembeza bidhaa au wenye meza ndogo za kupanga bidhaa pembezoni ya barabara Kariakoo.Wanashida na mtu anayeshusha Contena zima la bidhaa ,anaweka Katikati ya barabara alafu anajita Mmachinga.
Mh RC, Rais wetu mpendwa , wamachnga walipe kodi, maduka nao walipe kodi, fedha tunazo nyingi ni nyie tu mje kjuzikusanya.