Kariakoo ni kituo cha Uchuuzi cha Kimataifa, Sio kituo cha Biashara cha Kimataifa

Kariakoo ni kituo cha Uchuuzi cha Kimataifa, Sio kituo cha Biashara cha Kimataifa

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2020
Posts
4,548
Reaction score
11,901
Kariakoo ni sehemu ya kuchuuza vitu ya kimataifa na inapata promo kwa sababu pia tunazungukwa na nchi randlocked nyingi tunazo fanana nazo kama Burundi, Congo, Rwanda, Zambia, Malawi hizo zote ni nch za uchuuzi, za Frame Economy. Kariakoo haiwezi kuwa kituo cha Kibiashara cha kinataifa, kariakoo inaendehswa kiswahili sana, imejaa ushwahili.

Kariakoo Haiwezi kuwa kituo cha Biashara cha kimataifa, ilihali ukiwa na ratiba ya kwenda Kariakoo unaanza kuwaza utafika fikaje kule.Make hata kwa miguu kariakoo haiingiliki kirahisi kwa sababu ya kiwango cha uchuuzi.

Ustarabu ni negative pale Kariakoo.

Pale ndio shule kwa vijana wa Kitanzania kwenda kujifunza uchuuzi na kurudi kufungua frame mikoani huku.

Kariakoo haiwakikishi uchumi wa nchi kwa sababu pale asilimia 100 ya Products nu made ni nje, China na India na kwingineko huko.

Huwezi tamba kuwa na kituo cha biashara cha kimataifa ilihali asilimia 100 ya biadhaa pale ni imported, hii inawezekana kwa Taifa la wajinga kama Tanzania walio zoea kudanganywa.
 
Biashara zimefika hadi barabarani. Mkabala na kituo cha mwendokasi misimbazi karibu na total petrol station watu wanapanga bidhaa barabarani kabisa. Barabara za mitaa zote zimegeuzwa maduka ya wazi. Mtaa wa aggrey pale kutokea barabara ya Dart watu wanashusha mabalo ya nguo wanafungua na kuyafunga kisha kuyapaki tena. Yaani watu wanafanya biashara barabarani na serikali ipo tu!

Mtaa wa Congo haupitiki. Watu wameziba barabara. Kukitokea ajali itakuwa vigumu sana watu kujiepusha na maafa maana msongamano ni mkubwa unaotokana na kuziba barabara za mitaa ya kariakoo.
 
Nipo kariakoo zaidi ya miaka 12 lkn ukiniambia mara ya mwisho nilipita lini mtaa wa Congo sijui, kuna baadhi ya mitaa kariakoo kama hauna ishu nayo usipite kabisaa.
Kariakoo imekuwa ya hovyo na inazidi kuwa wajinga kutokana na utaratibu mbovu wa wafanyabiashara, bodaboda, daladala na magari ya mizigo
 
soko halina zones, limejaa machinga, wezi, boda boda, watu wa mizigo bila mpangilio kuna wale jamaa waokota chupa na mifuko yao pia wanafosi kupenya mashabiki wa simba na yanga nao ni uwanja wao wa mabishano kimsingi soko linahitaji maboresho ya hali ya juu kuanzia njia, miundo mbiu, mifumo ya taka, kuligawa soko kwa ZONES, na kuzia baadhi ya mambo ya kipuuzi
 
Kariakoo ni reflection ya uwezo wetu wa kupanga kama taifa.
kuwa kariakaoo ni sawa. A kuwa kwenye bahari iliyochafuka sana, ni kero kubwq sana, na watu wenye kupenda utulive ni nadra kuwakuta pale.
 
Kariakoo ni sehemu ya kuchuuza vitu ya kimataifa na inapata promo kwa sababu pia tunazungukwa na nchi randlocked nyingi tunazo fanana nazo kama Burundi, Congo, Rwanda, Zambia, Malawi hizo zote ni nch za uchuuzi, za Frame Economy. Kariakoo haiwezi kuwa kituo cha Kibiashara cha kinataifa, kariakoo inaendehswa kiswahili sana, imejaa ushwahili.

Kariakoo Haiwezi kuwa kituo cha Biashara cha kimataifa, ilihali ukiwa na ratiba ya kwenda Kariakoo unaanza kuwaza utafika fikaje kule.Make hata kwa miguu kariakoo haiingiliki kirahisi kwa sababu ya kiwango cha uchuuzi.

Ustarabu ni negative pale Kariakoo.

Pale ndio shule kwa vijana wa Kitanzania kwenda kujifunza uchuuzi na kurudi kufungua frame mikoani huku.

Kariakoo haiwakikishi uchumi wa nchi kwa sababu pale asilimia 100 ya Products nu made ni nje, China na India na kwingineko huko.

Huwezi tamba kuwa na kituo cha biashara cha kimataifa ilihali asilimia 100 ya biadhaa pale ni imported, hii inawezekana kwa Taifa la wajinga kama Tanzania walio zoea kudanganywa.
Ahsante kwa hili.

Moja ni “Landlocked” na pia kwa kweli hatuwezi sema ni Kituo cha Biashara cha Kimataifa ikiwa 99% ya bidhaa zinazouzwa pale ni bidhaa bandia (counterfeit goods). Katika hadhi za Kimataifa hilo tu linafanya tutolewe katika hadhi hiyo.
 
Back
Top Bottom