Muuzaji ana mafunzo gani ya kuuzia watu, muulize muuzaji analipwa kiasi gani kukidhi nauli, chakula, kodi, matibabu na ada ya mtoto wake chekechea.Walioajiriwa kwaajili ya kuuza ndo huwa wana tabia hizo ,lakini ukimkuta mwenye mali atakuhudumia vizur tu
Wenzetu wana karne na karne wanafanya hivi, babu zao wamejenga ukuta mrefu duniani unaoshangaza dunia hadi leo (maajabu ya dunia). Sisi hatuna utamaduni huo wa kufanya biashara zilizotukuka, wengi wetu tunatoka familia waganga wa kienyeji, wacheza ngoma, wachawi, wafugaji holela na kulima kwa kijembe cha mkono bila kutumia samadi hata kama ipo. Ghafla tukajikuta tunafanya biashara, tunadhani mteja atakuja tu kwa kuvutwa na dawa. Ukienda kule Tanga utakuta kwenye biashara kuna tula (ndulele) zile za njano, ukiuliza za nini watakujibu "wee acha tu watu sio wazuri". Watu kama hawa ukiwachanganja pamoja na wachina ambao hawaweki tula lakini wanauza sana lazima watajifunza jambo kwa kuona, kuambiwa au kwa kuiga.Mchina anajielewa
😂😂Umitashumta hiyohiyo mbona wakinga wanatoboa?, kule kwetu Tanga ukitumwa dukani lazima uende na shilingi Moja ya kugongea dirisha la dukani kumuita muuzaji aje akuuzie, maana hakai dukani lazima aitwe na mteja. Unagonga na kuita duuukaniiii, maduka wanafungua saa 3 asubuhi na kufunga saa 2 usiku.
Unacheka!!! Kule kwetu maduka yanafunguliwa saa 3 na kufungwa saa 2 usiku, yanafungwa kila muda wa kuswali unapofika unapoisikia adhana utadhani mji mzima ni waislam. Hivi akitokea mchina akafungua duka la unga wa dona na majani ya chai akawa anafungua kilasiku kuanzia saa 12 asubuhi na kufunga saa 6 usiku na kila ukienda dukani unamkuta na anatabasabu kwanini niende kwenye duka la mzawa? Huyu mzawa atadai kuwa wachina wanatuingilia kwenye biashara zetu ndogondogo? Yaani mimi nisinunue unga wa ugali kwakuwa wewe unaswali msikitini, khaaaaa!!
Safi sana unawakomesha, hata mm nafanya hi yo. Lakini hata sisi wateja tunachangia shida hii kwakuwa tuko tayari kusubiri mwenyeduka aje atuuzie bidhaa, yake tena unamwambia naomba chumvi na akikuhudimua unasema Asante.. na wakati mwingine unaenda kumuita aje akuuzieMimi nikiingia dukani na mwenye duka ameshika simu, naondoka
Iwe hata pharmacy au sehemu yoyote
Mteja bongo anaonekana kama zoba fulani hivi
Yaani huduma kwa wateja kwa nchi nyingi masikini ni zero kwa sababu hawafundishwi adabu shuleni wala nyumbani
Kuna dawa nilikuwa naitafuta pharmacySafi sana unawakomesha, hata mm nafanya hi yo. Lakini hata sisi wateja tunachangia shida hii kwakuwa tuko tayari kusubiri mwenyeduka aje atuuzie bidhaa, yake tena unamwambia naomba chumvi na akikuhudimua unasema Asante.. na wakati mwingine unaenda kumuita aje akuuzie
Safari yetu ni ndefu sana, kuwafukuza wachina mitaani kutatuchelewesha. Yaani unakula chakula kibichi kwakuwa tu kimepikwa na mkeo.Kuna dawa nilikuwa naitafuta pharmacy
Kuna moja waalikuwa wasichana wanne na wote wako kwenye simu wanachat
Niliwafokea na kuwaambia mnapoteza wateja kwa kiburi chenu
Je mwenye mali anajua?
Nikatoka zangu
Naweza kusalimia kwa sababu nimeingia sehemu
Ila kwa jinsi nilivyowakuta wana chat utadhani wanauza online
Sikuwa na mda hata wa kusalimia
Kwa kweli inaumiza sanaSafari yetu ni ndefu sana, kuwafukuza wachina mitaani kutatuchelewesha. Yaani unakula chakula kibichi kwakuwa tu kimepikwa na mkeo.
Kufanya kazi na kuhudumia watu vizuri kumegeuka ni utamaduni kwa baadhi ya watu na makabila na mataifa kutokana na watoto wao wamezaliwa na kukuta tabia hiyo kutoka kwa mababu, mabibi na wazazi wao.
Nyerere ndiye aliyetupoteza sisi. Wakati tunatafuta uhuru alitwambia tunatafuta uhuru ili kuondoka na kero za kulipa Kodi na unyapara. Baada ya kupata uhuru akafuta Kodi na unyapara hadi watu wakaaminishwa kuwa kulipa Kodi na kusimamia . ni ukoloni