Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
anza leo kutafuta chanzo cha mafanikio ya wakinga hapo kariakoo. Hao jamaa wanachana mbao utadhani wanachana mabua, kazi ambazo mzaramo sio tu hazitaki bali haziwezi pia. Biashara zetu sisi ni kuuza maembe aina ya mawazo na madafu kwenye mapakacha machafu na baiskeli kuukuu. Utamchukiaje mchina kama akiamua kuuza maembe ya mawazo kwenye kibanda kisafi kilichopigwa rangi chenye feni na kutumia vifungashio vizuri na kutabasamu wakati anakuuzia?huo muda wa kumchunguza mkinga we uliupataje?.
Wewe hujaelewa mada umekurupuka.Kariakoo wafanyabiashara wakubwa sio wachina ni wazawa ila tu mnadanganyana tu humu. Wachina wamezidi tu kidogo wafanyabiashara wa kati wa kawaida ila hakuna wachina level za Kina Gsm, Metl, Bakhresa na wengineo kwa sasa. Bado biashara kubwa kubwa ni za watanzania. Ushamba wetu tu kuwatukuza.
Wewe hujaelewa mada umekurupuka.
Hapa mada haiongelei ukubwa wa biashara ila mada inaelezea umahiri wa wageni kwenye kufanya biashara either iwe kubwa au ndogo.
Ukiona hao wakina Gsm wamefika level za juu ujue walikuwa na nidhamu kwenye biashara zao,ingekuwa wanafanya kienyeji tu bila kujua customer care na huduma nzuri wasingefika kwenye level hizo
Huo umahiri si ndio unafanya biashara iwe kubwa? Kuna wachina kibao biashara zinawashinda kkoo wanaondoka, mambo sio marahisi kama mnavyoyaongea,Wewe hujaelewa mada umekurupuka.
Hapa mada haiongelei ukubwa wa biashara ila mada inaelezea umahiri wa wageni kwenye kufanya biashara either iwe kubwa au ndogo.
Ukiona hao wakina Gsm wamefika level za juu ujue walikuwa na nidhamu kwenye biashara zao,ingekuwa wanafanya kienyeji tu bila kujua customer care na huduma nzuri wasingefika kwenye level hizo
Sasa kama wachina biashara zinawashinda kwa nini hao wafanyabiashara wa kibongo wanalalamika?Huo umahiri si ndio unafanya biashara iwe kubwa? Kuna wachina kibao biashara zinawashinda kkoo wanaondoka, mambo sio marahisi kama mnavyoyaongea,
Vituo vya ITV na TBC vilianzishwa miaka mingi sana kabla ya Azam TV, nini kimetokea kwa Azam tv kuwa kubwa kuliko ITV, Star TV na hata TBC?. Tutajikaanga wenyewe kama hata baada ya miaka 60+ ya uhuru bado tunakula maembe yaliyotandazwa chini kandokando ya barabara. Unaenda dukani kwa mtu unamkuta muuzaji amenuna na bei kamili za bidhaa hazifahamiki mpaka mjadiliane kwanza apunguze, na kweli anapunguza baada ya kupoteza muda wa kuomba kupunguziwa. Kama akikubali kupunguza bei maana yake alipandisha bei ya bidhaa hiyo.
Wafanyabiashara wetu ndio wanaoongoza kuingiza bidhaa hafifu kutoka china na kuja kuuza kwa bei kubwa, sio watu hawa. Bidhaa za china zinazoenda Asia, ulaya, marekani na hata Kenya hapo ni tofauti sana na bidhaa zinazoletwa tz na watu wetu wenyewe. Ni heri wachina walete wenye bidhaa zao hapa na wabongo tukafungashe kwao, hata serikali itakuwa rahisi kudhibi ubora na kodi. Sio kila mtu aende china na fedha kidogo sana na kuja na bidhaa nyingi hafifu hapa kwa bei ya bidhaa safi zenye uboraSasa kama wachina biashara zinawashinda kwa nini hao wafanyabiashara wa kibongo wanalalamika?
Uko sahihi,na hata wateja wa kibongo pia hawataki habari za bidhaa original hao wanataka bidhaa za bei rahisi tu hawataki kusikia wimbo mwingine.Wafanyabiashara wetu ndio wanaoongoza kuingiza bidhaa hafifu kutoka china na kuja kuuza kwa bei kubwa, sio watu hawa. Bidhaa za china zinazoenda Asia, ulaya, marekani na hata Kenya hapo ni tofauti sana na bidhaa zinazoletwa tz na watu wetu wenyewe. Ni heri wachina walete wenye bidhaa zao hapa na wabongo tukafungashe kwao, hata serikali itakuwa rahisi kudhibi ubora na kodi. Sio kila mtu aende china na fedha kidogo sana na kuja na bidhaa nyingi hafifu hapa kwa bei ya bidhaa safi zenye ubora
Watu wanalalamika wachina kufanya biashara zisizowahusu na sio kwamba wachina wanafanya biashara zaidi. Kila bidhaa unayo gusa hapa kkoo kuna wabongo kibao ndio wenye mitaji na mizigo mikubwa, atleast kwa circle yangu ya biashara.Sasa kama wachina biashara zinawashinda kwa nini hao wafanyabiashara wa kibongo wanalalamika?
Umesema vyemaNaenda dukani kununua kitu jitu linanijibu kwa dharau hatuuzi rejareja (Duka lenyewe halijakaa kijumla jumla). TF. Wachina washikisheni adabu mbuzi hao.
Kariakoo wafanyabiashara wakubwa sio wachina ni wazawa ila tu mnadanganyana tu humu. Wachina wamezidi tu kidogo wafanyabiashara wa kati wa kawaida ila hakuna wachina level za Kina Gsm, Metl, Bakhresa na wengineo kwa sasa. Bado biashara kubwa kubwa ni za watanzania. Ushamba wetu tu kuwatukuza.
Hata ulaya na marekani pia kuna wanaopenda vitu vya bei rahisi za clearance. Ndio maana bidhaa za china zimejaa kwenye maduka yao kwakuwa ni bora na bei rahisi. China wana quality aina zote za bidhaa, watu wetu wanatoa special order ya bidhaa za quality ya chini sana kuleta tz. Kuna aina ya Simu kutoka China zinapatikana kariakoo, huwezi kuipata Kenya hata Zanzibar; poor, poor,poor!!!Uko sahihi,na hata wateja wa kibongo pia hawataki habari za bidhaa original hao wanataka bidhaa za bei rahisi tu hawataki kusikia wimbo mwingine.
Watu wetu hawajui kufanya biashara, hawamjali mteja, hawajui kuweka kumbukumbu. Miaka 20 mtu amebaki kuwa machinga. Watu wetu wanapata uzoefu wa kuuza kutoka kwao. Kuwafukuza wachina na wageni tutawadumaza watu wetu na waendelee kutoa huduma mbaya kwa wateja
TFF iliporuhusu wachezaji 12 kwa timu Moja vijana wetu walipata uzoefu mkubwa kutoka kwa wageni. Kila golikipa sasa hivi anadaka kama Diara na Camara.
Utakuwa ujinga kama tutasema waondoke ili watu wetu wafanye hizo biashara, watakuwa machinga milele na kutoa huduma mbovu kwa wateja wao. Hata ukienda bar watu wetu hawajui kuwahudumia wateja wao.
Nimemulewa vizuri tu.Haujamuelewa mleta uzi
Sisi wateja (wanunuzi) tusipangiwe kabila la kutuuzia bidhaa, kama mchina atanikera kwenye biashara yake nitanunua kwa mmatumbi mwenzangu mimi mwenyewe. Hakuna biashara isiyomhusu mtu; biashara zote zinatawaliwa na kanuni ya soko ya demand, supply, price, customer care (hospitality) and 5s.Watu wanalalamika wachina kufanya biashara zisizowahusu na sio kwamba wachina wanafanya biashara zaidi. Kila bidhaa unayo gusa hapa kkoo kuna wabongo kibao ndio wenye mitaji na mizigo mikubwa, atleast kwa circle yangu ya biashara.
Naunga mkono hojaWatu wetu hawajui kufanya biashara, hawamjali mteja, hawajui kuweka kumbukumbu. Miaka 20 mtu amebaki kuwa machinga. Watu wetu wanapata uzoefu wa kuuza kutoka kwao. Kuwafukuza wachina na wageni tutawadumaza watu wetu na waendelee kutoa huduma mbaya kwa wateja
TFF iliporuhusu wachezaji 12 kwa timu Moja vijana wetu walipata uzoefu mkubwa kutoka kwa wageni. Kila golikipa sasa hivi anadaka kama Diara na Camara.
Utakuwa ujinga kama tutasema waondoke ili watu wetu wafanye hizo biashara, watakuwa machinga milele na kutoa huduma mbovu kwa wateja wao. Hata ukienda bar watu wetu hawajui kuwahudumia wateja wao.