Kariakoo tuwaache wachina watufundishe biashara

Hio ni opinion yako na iheshimiwe, ila si kweli kwamba wachina wanafundisha watu biashara, hapa sasa hivi kuna wachina wakiona uzi kama huu wanachekelea wanakusibiria wakubamize na bidhaa walizopiga winga.
 
Sasa kama Wabongo wanapiga hela zaidi ya Wachina kwa nini kumekuwa na malalamiko kwenye mitandao kuhusu ujio wa Wachina K/koo? Shida ni nini hasa?​
 
Naenda dukani kununua kitu jitu linanijibu kwa dharau hatuuzi rejareja (Duka lenyewe halijakaa kijumla jumla). TF. Wachina washikisheni adabu mbuzi hao.
Wakiona mwenzao wa pembeni wanauza watamwambia mchawi na wakiona wao hawauzi na pesa hawazioni utawasikia kuna chumaulete; kumbe shida ni wao wenyewe namna wanavyouza na kuhudumia wanunuzi na matumizi yao mabaya.
 
Naenda dukani kununua kitu jitu linanijibu kwa dharau hatuuzi rejareja (Duka lenyewe halijakaa kijumla jumla). TF. Wachina washikisheni adabu mbuzi hao.
Mwingine anakuambia sina change. Sasa unafanya biashara ya nini kama huna change. Yaani wabongo wengi hawajuagi kumjali mteja. Huduma kwa wateja hovyo.
 
Sasa kama Wabongo wanapiga hela kwa nini kumekuwa na malalamiko kwenye mitandao kuhusu ujio wa Wachina K/koo?​
Kuna malalamiko mengi JF kwa watu ambao hata kkoo hawajafika kushinda hao wafanyabiashara kkoo.

Watu wanalalamika wachina wanafanya biashara zisizowahusu mfano kupiga winga, Mchina anatakiwa aje na mtaji toka kwao afanye uwekezaji na sio kuja na nguo zake na kununua Kilichopo hapa na kukiuza.

So huu ni mtifuano wa wafanyabiashara wadogo design ya machinga ama wenye vigoli na Wachina wasio na mitaji, ita has nothing to do with Wafanyabiashara wa kawaida kkoo ama wachina wenye mitaji.

Kihaki kabisa hawa Machinga na hao wachina Mawinga wote hawakupaswa kuwa kkoo wakatafutiwe tu vigoli vyao machinga Complex huko.
 
Hapo kwenye kusaidia ndugu zake, yupoje, anasaidia au hasaidii
 

Wasifukuzwe, ila tuangalie namna bora ya kuwatambua na kuwasimamia wafanye biashara kwa msingi wa sheria zilizopo. Hii itawasaidia wachuuzi wetu wawe na uwezo kama wa wachina. Kama mchina ana mtaji, na anataka muungane na mzawa kufanya biashara, hiyo ni ruksa. Itaongeza tija katika ufanyaji biashara wa watu wetu.
Ila sasa wachina ni wa kuwaangalia sana. Wanazaa hovyo hovyo na vibinti vyetu. Yaani tumeanza kuona vijukuu vya mchanganyiko na vichina kila kona. Sasa sijui wanataka tuwe ndugu kwa lazima!!!???
 

Acha waje mpaka akili zetu zifunguke. Wabongo tumezoea sana paradiso ya kufikirika. Hatutaki kujituma, hatutaki ubunifu, hatutaki kujitesa tunataka kila kitu kije kama mvua. Hakunaga maisha ya hivyo. Zamani nilikuwa nawachukia wanyang'au, acha nao waje tupige kazi hapa.

Watu wanalia lia, lakini kule katavi kuna wakenya wengi tu wanapiga mishe. Kitu ambacho ni kizuri. Pigeni misheee, kulia lia hakuna faida
 
Hilo la kuzaa hovyo hovyo nani alaumiwe? Kama binti ana miaka zaidi ya 18 akizalishwa kapenda mwenyewe.
 
Kwa hiyo wafanyabiashara wakubwa wa K/koo suala la ujio wa Wachina haliwaumizi?​
 

acha kupenda mteremko mkuu, Kariakoo vitu ni bei rahisi sana kwa maana ya sana. kama unataka rahisi zaidi ya hapo si bora upewe bure tu.
 
Kwa hiyo wafanyabiashara wakubwa wa K/koo suala la ujio wa Wachina haliwaumizi?​
Haliwaumizi sana na naweza kusema wengine wanafaidika zaidi. Mtu yoyote anaekujua China na anaweza kuleta kontena lake hasumbuliwi na wafanyabiashara wa kichina Kkoo.

Wabongo wengi wanaokwenda China bidhaa zao ni rahisi zaidi kushinda za wachina, atleast kwa hao wafanyabiashara wakubwa.

Niliwahi toa mfano Gsm humu, toka alete brand yake ya Zanzibar Textiles kuanzia mashuka, Maduvet na vifananiavyo kakimbiza wachina kibao kkoo, kila duka unalokwenda ni bidhaa zake,
 
Kwa hiyo Wachina waendelee kuchapa kazi K/koo?​
 

Mkuu jamaa sio watu wazuri, hizo zote ni strategy. Wakishizaa na mbongo ndio ameshapata uhalali wakuishi na kumiliki mali kwa kupitia mgongo wa familia. hawa jamaa wana target kubwa sana za mbali. acha wabongo washerekee kuuziwa jeans bei chee na mchina huku tukisubiri wachina kufikia malengo yao ambayo sote kwa pamoja tutakuja kulia mbeleni
 
Ni rahisi hivyo kupuuza kazi na tafakuri ya wanatume juu ya kadhia dhidi wafanyabiashara walio wengi na maslahi mapana ya taifa. Sio Kila Jambo linamfanano na futiboli.
 
Hapo kwenye kusaidia ndugu zake, yupoje, anasaidia au hasaidii
kila ndugu anajipambania hadi tone lake la mwisho, utegemezi sio mkubwa kama makabila mengine. Ona wahindi, wote wanabanana pale upanga kwenye nyumba hizohizo ili kubana matuzi; faida iwe kubwa. Mswahili anajenga nyumba kwa biashara ya umachinga miaka 10 badala ya pesa hiyo kutumika kama mtaji wa kuisogeza biashara yake level nyingine. Na akishamaliza kujenga hiko kijumba basi matangazo ni kila kona "nimejengaaaaa" na ndugu zake wote toka kijijini wanahamia kwake kuishi kwa mjomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…