Kariakoo tuwaache wachina watufundishe biashara

Hiyo ya kununua dollar ni habari nyingine, sio ya kariakoo. Idara ya fedha ifanye kazi yake. Mimi nilikuwa Addis Ababa, kule ni vigumu kupata dola, wanakupa hela yao (Bir) uitumie pale, kama hutaimaliza kule utarudi nayo tz. South Africa hivyohivyo huwezi kupata dola kirahisi, utachezea rand yao weee hadi unarudi hapa.
 
mwenzako mwenye mtaji akitembea wewe kimbia.
Sio kwa mtizamo wako. Ngoja nikusidie kidoogo japo sio sana utanielewa. China wao wanachukua mkopo bank kwa single digital. Yaan kwa asilimia 3. Sisi huku kwetu tunachukua mkopo kwa asilimia 19 mpaka 30 we kwa akili yako unaweza kushindana na huyo mtu sokon?
 
Shida hapo sio wachina bali ni wafanya maamuzi wetu.
 
Soko limejaa mawinga kibao unategemea nini. Yaani muuzaji halisi hajulikani.
 
Wengi sana wapo hivi, mara nyingi huwa najiuliza kwani hii huduma au bidhaa yake ni free au nalipia.

Bongo customer care ni mbovu siyo kwenye biashara tu bali hadi kwenye idara/taassisi za serikali.

Niliona hili NSSF wiki jana.
 
Mikopo ya kausha damu. Kote hadi Ulaya mkopo hauzidi 3% riba. Wanatushangaa tunawezaje kuinuka kiuchumi kwa mikopo hii.
 
Wengi sana wapo hivi, mara nyingine nyingi huwa najiuliza kwani hii huduma au bidhaa yake ni free au nalipia.

Bongo customer care ni mbovu siyo kwenye biashara tu bali hadi kwenye idara/taassisi za serikali.

Niliona hili NSSF wiki jana.
Siku moja niliwatolea mbovu pale MOI, mgonjwa kapata huduma vizuri pale kitengo cha dharura na kuletwa MOI wodini. Wale wahudumu uchwara wako busy wanajaribisha makoti huku mgonjwa anapigwa na baridi. Niliwawakia . Kuna watu walikuwa pale toka saa tisa mchana eti mpaka saa sita usiku wagonjwa wao hawajapelekwa wodini.
 
Kiukweli nchi yetu bado sana kwenye huduma kwa wateja halafu wakiwa kwenye hizo nafasi wanahisi washamaliza kila kitu.
 
Si justify ila hili tukio limetokea last two weeks Mbeya,same as you.
Nimevaa kobazi zangu na kama ujuavyo wanaume hatuna mambo mengi,kila ukuuliza wanakushusha wanakupandisha,nilihisi nimekosea duka ile siku.
Nilijisikka vibaya sana,bahati mbaya simu ikaita mfukoni ile naitoa ikanguka na funguo😀aisee hali ya hewa ilibadilika pale ndani,wakaanza boss wanatoa hiki wanatoa kile,kwa jinsi nilivyokuwa treated awali niliondoka nikaenda kwa jirani .

Mwenye duka namjua,ilibidi jioni nimpigie nimwambie,wafanyakazi wako wanaharibu biashara yako nzuri mrembo wangu.
 
Kenya ipi unazungumzia?
 
Wengi sana wapo hivi, mara nyingine nyingi huwa najiuliza kwani hii huduma au bidhaa yake ni free au nalipia.

Bongo customer care ni mbovu siyo kwenye biashara tu bali hadi kwenye idara/taassisi za serikali.

Niliona hili NSSF wiki jana.
CCM kuendelea kuwepo madarakani hadi Leo Kuna uhusiano mkubwa na hiki unachokiona kariakoo na kwenye taasisi ya serikali. Serikali haitaki kuwaudhi watu kwa kuwambia kile kinachopaswa kuambiwa, maana wanazihitaji kura zao. Na pia wanaujua sera zao ndizo zilizowafikisha watu hapo walipo na vile wanavyofanya. Ni vicious cycle kaka ya nyani haoni kundule. Mwalimu alifundishwa kama vile na yeye anafundisha kama vile.
 
Kama wachina wanakopa kwa riba ya 3% wakati watz wanakopa kwa riba ya 30% nani alaumiwe, wachina wa kariakoo?
Wanakopa kwao sio kwetu. Kwenye benk zao. Pili wana access ya kuaminiwa na viwanda vyao kupitia udhamini wa serikali zao. So wanapata ile bei ya firs class. Mi napata bei ya mtu wa tatu kufikia wa mwisho. Tatu wachina wamesambazwa dunian kote kwa mission maalum kimkakati.
 
Uliwaonea tu. Waulize mishahara wanalipwa Bei gani. Hicho wanachofanya kinalingana na kiasi wanacholipwa. Huwezi kutegemea huduma Bora kutoka kwa mtu ambae hana Raha na kazi yake. Mshahara haufiki tarehe 10 ya mwezi huohuo, hajui atakula nini mchana kazini, hajui nauli atapata wapi ya kurudia nyumbani. Mwajili wake hajui mtumishi wake anaishi wapi na na kula nini akiwa kazini. What do you expect?. Shida yetu sisi raia tunaelekeza lawama zetu sehemu zisizo sahihi kama wachina na watumishi, badala ya kuelekeza malalamiko kwenye route causes (mizizi) ya tatizo.

Katika nchi maskini hivi yenye huduma mbovu kama hizi hutarajii kuona Rais mstaafu akiwa na majumba makubwa mengi na utajiri mkubwa, aliupataje wakati hali ya nchi ni mbaya?:Mnataka kuwatoa macho wachina na watumishi bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…