Pendragon24
Member
- Aug 8, 2018
- 73
- 109
Kwa nini Serikali isiajiri wageni Serikalini pia kwenye ajira ili watanzania tuhudumiwe vizuri kwa maana watanzania wenzetu kwenye mashirika ya uma wanatuhudumia kwa kujivuta kama vile wanalazimishwa?.Hawa jamaa zetu kutoka Pemba, Njombe, Kigoma, Kilimanjaro n.k waliopo Kariakoo hawataki kabisa kusikia tunanunua bidhaa kwa bei nafuu na kufanya maisha yetu yawe magumu kidogo.
Wao wanawaza kutupiga bei kubwa kwa kisingizio cha uzawa na uzalendo uchwara, wakati wateja wanunuzi raia wa kawaida tunataka unafuu wa maisha na bei za bidhaa
Wachina wasiishie tu kaliakoo bali waajiriwe kwenye sekta za uma na Serikalini pamoja na sekta binafsi Ili waongeze ufanisi na kutufundisha namna ya kufanya kazi kwa ubora bila kulalamika lalamika.Sasa kama Wabongo wanapiga hela zaidi ya Wachina kwa nini kumekuwa na malalamiko kwenye mitandao kuhusu ujio wa Wachina K/koo? Shida ni nini hasa?
Wapewe kabisa na ajira Serikalini/sekta binafsi hata kazi zile zinazoweza fanywa na wazawa Ili kuongeza ushindani wakutoa huduma nzuri kwa wananchi.mimi sioni tatizo wachina kuishi nchini na kufanya shughuli zao za kujitafutia kipato. cha muhimu ni kuwa wasivuruge mfumo wa njia za vipato vya wananchi.
Wapewe pia ajira na Serikali Ili ukienda kote huko uhudumiwe vizuri.Sijui biashara lakini najua kuhudumiwa vizuri.
Wapumbavu ni wengi mkuu hawawezi kuelewa . Wambie hao wachina/wahindi wapewe na ajira kabisa Serikalini Ili watie akili.Sio kwa mtizamo wako. Ngoja nikusidie kidoogo japo sio sana utanielewa. China wao wanachukua mkopo bank kwa single digital. Yaan kwa asilimia 3. Sisi huku kwetu tunachukua mkopo kwa asilimia 19 mpaka 30 we kwa akili yako unaweza kushindana na huyo mtu sokon?
Wapewe kabisa na ajira Serikalini/sekta binafsi hata kazi zile zinazoweza fanywa na wazawa Ili kuongeza ushindani wakutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Ukisema hivyo wapumbavu wengi wataona sio sawa kwa sababu ya uhaba wa ajira. Lakini haohao wanaona ni sawa wachina kufanya uchuuzi wakati wameingia kama wawekezaji.kama ni hivyo basi wangeanza kupewa serikalini.
Wachina wasiishie tu kaliakoo bali waajiriwe kwenye sekta za uma na Serikalini pamoja na sekta binafsi Ili waongeze ufanisi na kutufundisha namna ya kufanya kazi kwa ubora bila kulalamika lalamika.
Hapo nadhani itakua bora zaidi au mkuu unasemaje?.
Kwa nini Serikali isiajiri wageni Serikalini pia kwenye ajira ili watanzania tuhudumiwe vizuri kwa maana watanzania wenzetu kwenye mashirika ya uma wanatuhudumia kwa kujivuta kama vile wanalazimishwa?.
Hao akina METL, GSM, Azam achana nao kabisa, biashara ni asili yao tangu enzi na enzi, wamerithi tabia, misingi na wateja wa biashara zao Toka kwa mababu zao.Hao Akina METL, BAKHRESSA na GSM sio watanzania, hata kama ni Watanzania ni Uraia tu lakini sio NYANI
NYANI Hawawezi biashara, wanaweza Nyodo na Uchawa
Hiyo ni ego inamsumbua yeye haamini kuwa watu wengine hawawezi wakahaso na wakatoboa na wakafika levo za juu kumpita yeye Bali atajifariji kuwa akaiba, akaroga, freemason,akapata zali nk Sasa njoo yeye akifanikiwa atajisifu kuwa mie ni mjanja nimekesha ,nimekomaa mno,nimeshindia mkate na maji,nimelala stendi nk.Hiyo sio kweli, nenda kamchunguze mkinga uone anaamka saa ngapi kufungua biashara na anafunga saa ngapi na anawahudumiaje wateja wake. Chunguza matumizi yake na anakula nini na kiasi gani kwa siku. Mchunguze uone kama ana roho nzuri ya kusaidia ndugu zake na kunywa pombe na starehe nyingine za wanawake, chunguza kama anafiwa uone kama anafiwa na kuhudhuria misiba Kila siku, nenda kaone namna anavyoongea na mteja wake na usafi wa bidhaa yake, hakuna uchawi kaka anajilipua TU na kufuata misingi ya biashara. Wewe Kila siku uko kipalang'anda kuzika mjomba mara kaka yake mdogo mkazamjomba mara rafiki yake wa utotoni mdogo wake bibi Yako.
Biashara ni mapato na matumizi
Hata ukitoa hao kuna wachaga na wabongo wengine kibao hapo kkoo, ukiwa hupo kwenye Inner circle haya mambo huwezi kuyaelewa.Hao Akina METL, BAKHRESSA na GSM sio watanzania, hata kama ni Watanzania ni Uraia tu lakini sio NYANI
NYANI Hawawezi biashara, wanaweza Nyodo na Uchawa
Hawajaliteka, huwezi kuteka soko kwa kuwa na kifremu kimoja tena unauza reja reja.So unavyo fikiri soko bado hawajaliteka ama tayari?
Paka ni paka rangi ya paka haisaidii kwenye kukamata panya. Mimi mlaji wa mwisho nahitaji kilicho bora kabisa, nahitaji kujaliwa na kuheshimiwa pale ninapokweta kuspend my money. Mimi siko pale kupewa huduma mbovu eti kwakuwa inatolewa na mchaga au mzaramo mwenzangu.Hizi ni akili za KITUMWA mno hata wakina TIP TIP walifikiri hivi hivi kuhusu watanganyika wenzao wakashirikiana na explorers wakawafanya watumwa.
Ashukuriwe Mwl Nyerere🙏
Machinga halipi Kodi lakini hana lugha nzuri pia. Riba ya Mkopo ina uhusiano gani na lugha nzuri kwa mteja wako?Wapumbavu ni wengi mkuu hawawezi kuelewa . Wambie hao wachina/wahindi wapewe na ajira kabisa Serikalini Ili watie akili.
Maana wanaona kama wafanyabiashara wanalalamika bure, wanataka faida kubwa. Lakini wanasahau mabank ya bongo ukikopa riba ni asilimia 17/20. Wakati huko china riba ni asilimia 2/4. Sasa watu Hawa wakipewa mkopo sawa unadhani watauza Bei Moja Ili waweze kupeleka rejesho?.
Pia wao wachina wanaingia kama wawekezaji na wanapewa grace period ya kulipa kodi, huku wewe mzawa ukianza tu biashara Kodi ni lundo kutoka Serikalini.
Waajiri wachina/wahindi Serikalini Ili wahudumie watanzania kwa lugha nzuri, Kama watanzania tunalugha mbaya Kila mahala tujaze wageni.Machinga halipi Kodi lakini hana lugha nzuri pia. Riba ya Mkopo ina uhusiano gani na lugha nzuri kwa mteja wako?
Sasa mbona Rwanda Iko nyuma kiuchumi licha ya kuajiri hao wageni Tena nyadhifa za juu, nilitegemea iajiri wageni kwenye nafasi zinazoweza fanywa na wanyarwanda nafasi za kawaida tu sio huko kwenye managerial position. Wawaajiri ngazi ya officer/assistant officer kwenye mashirika ya uma huko Rwanda.Soma :
Taasisi nyeti nchini Rwanda sasa zaongozwa na Wataalamu kutokea Ulaya, Marekani na Israel
Taasisi nyeti nchini Rwanda ikiwemo mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii sasa inaongozwa na Wataalamu wa kigeni. • Christopher John Wales (Uingereza) Mwenyekiti wa Rwanda Social Security Board (RSSD) •Philipe Watrine (Uingereza) Naibu Mkurugenzi Mkuu anayesimamia uendeshaji wa Mfuko...www.jamiiforums.com
Soma :
22 March 2025
WAZIRI AWESO AMPA RAIS SAMIA KISA cha INJINIA ALIYE MBANANISHA AKASEMA WANAKIJIJI WACHAWI - MABOMBA YANAPAA
View: https://m.youtube.com/watch?v=3EAdMyh2c2U
Mhindi ukienda dukani kwake atakwambua karibu dugu yangu, mwarabu atakwambia salamaleku karibu, mchaga atakwambia karibu boss, mzaramo na mkwere watakwambia nini?Waajiri wachina/wahindi Serikalini Ili wahudumie watanzania kwa lugha nzuri, Kama watanzania tunalugha mbaya Kila mahala tujaze wageni.