Kariakoo tuwaache wachina watufundishe biashara

Kijana sichukii hizo jamii ila naweka uwazi mambo yao tu.
 
Tuko chini ya miti tunalalamika! Hatutaki uza karanga wala bidhaa ndogo ndogo ka hizi! Kisa tumesoma chuo kikuu! Wavivu, wadanganyifu, wezi, waongo, twapenda rahisi rahisi, udini, mila na desturi zinazidisha umaskini wetu! Hata tukisoma twashindwa kutekeleza zile theories ziwe practical! Kulalamika, kutafuta visingizio, ujuaji!
Mchina kazi kazi!
 
Kijana sichukii hizo jamii ila naweka uwazi mambo yao tu.
Tafiti zote zinaonyesha kuwa kukosa ushindani kunadumaza kitu chochote kuendelea. Competition is the spice of Life. Hata mtoto mdogo ukimpakulia chakula kwenye sahani Moja pamoja na wenzake atachangamka kwenye kula, la sivyo hatashiba. Hata akili yake itachangamka haraka kuliko kumpa chakula cheke kwenye bakuli lake mwenyewe.
 
dah nahapo ni vijakaz sasa, wanajikuta wamefka aise.
Ila hko ni kufukuza wateja kweny biashara za watu.
 
Wengi sana wapo hivi, mara nyingine nyingi huwa najiuliza kwani hii huduma au bidhaa yake ni free au nalipia.

Bongo customer care ni mbovu siyo kwenye biashara tu bali hadi kwenye idara/taassisi za serikali.

Niliona hili NSSF wiki jana.
kabxa mkuu imagine unaenda hosptal manes wanasukana mda huo mwenzao anafolen kubwa kisa wao kitengo tofaut
 
So long as wapo kihalali nchini acha wafanye shughuli zao sambamba na watanzania wengine. Hata huko nje wabongo na waafrika kwa ujumla wanafanya shughuli zao bila shida yeyote so long wameingia kihalali hizo nchi. Biashara ni ushindani.
 
kabxa mkuu imagine unaenda hosptal manes wanasukana mda huo mwenzao anafolen kubwa kisa wao kitengo tofaut
Ukiona eanasukana wakati wa kazi maana yake hiyo kazi haitoi majibu ya maswali yao yote kwa kiasi kikubwa. Lazima majibu mengine wakayatafite nje ya kazi ile. Wajapani Wana kanuni yao ya kazi inasema kazi yoyote lazima ikamilishe malengo ya mfanyakazi na mfanyakazi lazima akamilishe malengo ya mwajili wake (kanuni Z), resprocal. Less pay and motivation is compounding uvivu na uzembe wa watu wetu kazini (kwenye ajira). Lakini inashamgaza kuona hata watu waliojiajili wenyewe kuwa wavivu na watu wasiowahudumia vema wateja wao.
 
hapo tuseme wote wanakauvivu tu walojiari na walio ajiriwa nao kisingizio ujira mdogo
 
hapo tuseme wote wanakauvivu tu walojiari na walio ajiriwa nao kisingizio ujira mdogo
Kuna wakati lazima waajili wote wakutane sehemu pamoja waajiliwa wao wapange kima cha chini cheye uhalisi kinacholingana ni mfumko wa bei kwa mfanyaki mwenye mke na watoto 4. Maana serikali inatambua watoto 4 TU. Kwahiyo mfanyakazi mwenye watoto wanne anapaswa kulipwa ujira kiasi gani? Na je, huyu mfanyakazi afanye nini na nini na nini ili alipwe mshahara huo?
 
unamaanisha sekta binafs ama?
 
Walioajiriwa kwaajili ya kuuza ndo huwa wana tabia hizo ,lakini ukimkuta mwenye mali atakuhudumia vizur tu
 
unamaanisha sekta binafs ama?
sekta zote, lakini hasa sekta ya umma ambayo ndiyo inayokusanya kodi zetu zooote. Yaani serikali iseme wakati inapanga kumpa mshahara ule askari polisi, mwalimu, mhasibu, muuguzi, daktari au mfanya usafi huwa wanazingatia nini na kutarajia nini kutoka kwa mtumishi. Kama take home ya polisi ni sh. 600,000, hii hela walizingatia nini na kutarajia atoe huduma yenye ubora gani. Katika kanuni ya utoaji huduma inamtaka mtoa huduma awe "whole fit", holistic approach yaani mtoa huduma awe tayari kimwili, kisaikolojia, kijamii (socially) na spiritually. Kama mzazi hujaacha pesa ya kutosha nyumbani huwezi kushangaa kusikia mtoto wake kaenda kula kwa jirani au ameiba andazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…