farasi6453
Senior Member
- Sep 26, 2022
- 100
- 101
Salamu wanajamvi. Mimi ni mkazi wa miaka 25 hapa Kariakoo. Pamoja na kero nyingi za kuishi hapo hususan wamachinga,uchafu, msongamano n.k kumeibuka kero mpya ya uchafuzi wa mazingira kwa kutumia spika zenye sauti kali inayofanwa na baadhi ya wahubiri katika kona za mitaa.
Kelele hizi wakati mwingine huanzia asubuhi hadi mchana
na wakati mwingine mchana hadi jioni.
Athari zinazotokana na hii ni kama ifuatavyo.
1-Biashara kuathirika kutokana na watu kutokusikilizana.
2-Mawasiliano kwa simu hamsikilizana kabisa.
3-Afya ya watu wazima na watoto kuathirika na sauti kali.
4-Watoto kukosa amani wakati wa masomo ya jioni nyumbani.
Habari kubwa ya sauti hubiri hizi ni kuomba michango kutoka kwa wapita njia.
Tunashangaa vyombo husika kama Halmashauri ya Jiji, Watu wa mazingira NEMC na TRA (Pesa inakusanywa kwa TIN ya nani) kukaa kimya kwa mda mrefu.
Naomba mamlaka inayosimami vyombo husika kuliangalia tatizo hili.
Asanteni.