Nimejaribu kutafiti katika mazingira tofauti kusikiliza katika vyombo vya habari kusoma magazeti kuwauliza watu na shahidi mbalimbali kutoka kwa marafiki zangu lkn wakati mwingine kuona kwa macho nikagundua kuwa karibu asilimia 90% hawafurahii ndoa za wengine mpaka kuona kuwa ndoa ni kama mzigo mkubwa kwao mpaka wanatamani kujitoa. Na utakuta wengine mpaka wanasema wasinge kuwa watoto ninge ondoka, lkn pia wengine wanavumia mateso masimango kwasababu tu wamejenga nyumba kubwa hawezi kuacha au wana magari maduka pesa hawezi kuondoka hata km ananyanyasika. Sasa naomba wana JF tuambizane ukweli hapa nini chanzo cha wanandoa walio wengi sio wote kutofurahia ndoa zao? wapo ambao wanauana ktk ndoa wapo wanaofumaniana wapo wanaopigana wapo wanao achana wapo wanaosalitiana wapo wanaologana wapo ambao hawaongeleshani japo wanakaa nyumba moja wa mzungu wanne ndo usipime. kila siku vurugu tu je? nini sababu ya ndoa kuwa ndoana? karibu kwa mchango wenu wa mawazo.