Katika huu uzi ebu tujuzane baadhi ya changamoto na migogoro ya ardhi hasa mipaka na majirani au jirani uliyepakana nae katika kiwanja chako, Ilikuwaje na mgogoro uliisha vipi.
Katika huu uzi ebu tujuzane baadhi ya changamoto na migogoro ya ardhi hasa mipaka na majirani au jirani uliyepakana nae katika kiwanja chako, Ilikuwaje na mgogoro uliisha vipi.
Migogoro mingi inatokana na ubinafsi na tamaa tu. Mtu anataka apande fensi au miti mpakani, akiambiwa aache hatua moja anaona eneo lake litapungua. Kuna mmoja amepanda miti yake, hapa nasubiri wakati wa kujenga ukuta, ataing'oa tu! Ni mbishi sanaa.
Kuna jirani wao wanagombea mti wa mparachichi, ulipandwa mpakani. Tawi moja liko upande wapili ila wa upande mwingine hataki mwenzake achume matunda. Ni balaa!