Jumbe Kondo
Senior Member
- Oct 18, 2011
- 109
- 68
- Thread starter
-
- #81
Mm nataka kwenda lamu,naomba utaratibu na gharama zakufika na kuishi huko ukoje,je huduma za kijamii kama hotel za kawaida na vyakula umekaaje,naomba majibu kwa kwenye uwelewa wa lamu
Naam zote zipo. Nitawapa hoteli na bei.Wazuri aisee....vp mkuu vyumba vya wageni huko bei zikoje?
Mfano, nikija nataka kuspend bila kumkera mtu...ntaweza pata night clubs na pombe?
Aiseee hii sehemu nikijaliwa uzima lzm niitembeleUkiwa Dar au Tanga au hata Arusha panda Tahmeed au Modern Coast ya moja kwa moja.
Ukifika Mombasa gari litavuka kwenda ng'ambo ya pili likitumia kivuko. Mtalipanda temna ng'ambo ya ili..kuna sehemu ya abiria kuketi kwenye kivuko.
Mombasa hadi Lamu takribani masaa matano.
Mtapita mitaa ya Mombasa kama Nyali (mtakapo vuka daraja), Kisauni, Bamburi, Shanzu, Shimo La Tewa halafu Mtwapa, Mnarani, Kilifi, Watamu, Mida, Malindi, Mambrui, Marafa, Witu, Hindi, Mokowe kisha mtapanda dau au motaboti kuwafikisha kisiwani.
Uingiapo tu hii, kuna mahoteli mazuri sana ufuoni na katika mitaa ya ndani.
Keshoye waweza funga safari kwenda Shela uzunguni au visiwa vyengine kama Manda, Manda toto, Pate, Kiwayuu, Faza ila utatumia dau au motaboti.
Kuna sherehe ningi sana kisiwani zenye mihemko na raha ya kutosha kama Maulidi, Tamasha la kiUtamaduni Lamu, mashindano ya punda kukimbia, mashindano ya ngalawa baharini n.k.
Vyakula na migawhawa murua vinapatikana kila sehemu.
Watu ni wakarimu.
Sehemu zengine za kutembelea ni maeneo ya MaliAsili naa Turathi za Kitaifa kama Ngome ya Lamu, Posta ya Mjermani, Misikiti ya Kale, Magofu ya tangu karne ya 8, hifadhi za Boni na Arawale, bahari ya hindi ukitumia motaboti.
Kuna ujenzi mkubwa sana unaoendeea kwa sasa wa mradi wa LAPSSEt ambalo linaanzia Lamu. Kuna bandari, reli, barabara za kimataifa, miundombinu ya stima, mambomba ya gesi na mafuta, mkonga wa mtandao, miradi ya mkaa na stima ya mawimbi na upepo n.k. Pia kuna uchimbaji wa gesi na mafuta baharini mbali na kitega uchumi maarufu cha Utalii.
Kwa hivyokuna fursa tele.
kwa watalii, huu ndomji wa kale zaidi wa Waswahili na uliohifadhiwa vyema. Kwa hiyo ukitaka kuwaona na kuwajua Waswahili halisi, maongezi yao, vyakula, tamaduni, samani, nyumba, makazi, hali ya maisha, nyimbo, mashairi, goma n.k. karibu ujionee na ufurahie mandhari kabla maendeleo ya kisasa hayajaugeuza mji kabisa.
Ukanimara mzee, adigo mara kukohiko mijikenda machiingira tanzania, nkweli asiliyehu yalakuko kwa arume amazu akaurika kayambaUkiwa Dar au Tanga au hata Arusha panda basi la Tahmeed au Modern Coast ya moja kwa moja kwenda Mombasa/ Malindi/ Lamu.
Ukifika Mombasa gari litavuka kwenda ng'ambo ya pili likitumia kivuko. Mtalipanda tena ng'ambo ya pili..kuna sehemu ya abiria kuketi kwenye kivuko/ feri.
Mombasa hadi Mokowe, Lamu takribani masaa masita. Motaboti kutoka jeti la Mokowe hadi la Lamu kwenye motaboti takriban dk. 15-30.
Mtapita mitaa ya Mombasa kama Nyali (mtakapo vuka daraja), Kisauni, Bamburi, Shanzu, Shimo La Tewa halafu miji mingine kama Mtwapa, Mnarani, Kilifi, Watamu, Mida, Malindi, Mambrui, Marafa hadi Minjila mtakapoliacha barabara ya kwenda Garsen-Galole-Hola-Bura-Garissa. Hadi hapa bararabara ni kiwango cha lami. Hapa panaitwa Tana Mtoni.
Kuanzia Minjila mtaenda kulia kupitia Idsowe. Hii barabara ni ya mchanga ila sio mbaya na inatengezwa lami sasa. Njia itawapeleka Witu, Mambosasa, Hindi hadi Mokowe. Hapa mtapanda dau au motaboti kuwafikisha kisiwani Amu.
Uingiapo tu hivi, kuna mahoteli mazuri sana ufuoni na katika mitaa ya ndani.
Keshoye waweza funga safari kwenda Shela uzunguni au visiwa vyengine vya kihistoria kama Manda, Manda toto, Pate, Kiwayuu, Faza ila utatumia dau au motaboti.
Kuna sherehe nyingi sana kisiwani zenye mihemko na raha ya kutosha kama Maulidi, Tamasha la kiUtamaduni Lamu, mashindano ya punda kukimbia, mashindano ya ngalawa baharini n.k.
Vyakula vya mtaani vipo na migahawa murua zinapatikana kila sehemu.
Watu ni wakarimu na wepesi wa kukusaidia na kukuelekeza.
Sehemu zengine za kutembelea ni maeneo ya MaliAsili naa Turathi za Kitaifa kama Ngome ya Lamu, Posta ya Mjermani, Misikiti ya Kale, misitu ya visiwani, Magofu ya tangu karne ya 8, mbuga za Boni na Arawale, bahari ya Hindi ukitumia motaboti.
Kuna ujenzi mkubwa sana unaoendeea kwa sasa wa mradi wa LAPSSET ambalo linaanzia Lamu. Kuna bandari, reli, barabara za kimataifa, miundombinu ya stima, mabomba ya gesi na mafuta, mkonga wa mtandao, miradi ya mkaa na stima ya mawimbi na upepo n.k. Pia kuna uchimbaji wa gesi na mafuta baharini mbali na kitega uchumi maarufu cha Utalii.
Kwa hivyo kuna fursa tele za ajira, biashara na huduma nyenginezo.
Kwa watalii, huu ndo mji wa kale zaidi wa Waswahili na uliohifadhiwa vyema. Kwa hiyo ukitaka kuwaona na kuwajua Waswahili halisi, maongezi yao, vyakula, tamaduni, samani, nyumba, makazi, hali ya maisha, nyimbo, mashairi, goma n.k. karibu ujionee na ufurahie mandhari kabla maendeleo ya kisasa hayajaugeuza mji kabisa.
Pia wamo Wabajuni na Wabarawa ( ni makabil ay ajadi ya Waswahili hawa ila wana utofauti kidogo), Wapokomo na wamo pia Watu wenye ukaribu na wa Khoisan ( Sandawe/ hadzabe) waitwao wa Boni au Arawale, wamo wasomali na pia makabila mengine ya Kikushi kama Waorma, Wawardei n.k. ambao asili yao ni Ethiopia. Wamo pia Wamijikenda ambao Wadigo ni wamoja ya miji yao ila huku kaskazini ndugu za Wagiriama ndo wengi zaidi. Lugha yao ni karibu mno na Kidigo.
Ila ustitie hofu killa mmoja yuaongea Kiswahili kisafi cha Lamu chenye ladha ya mashairi na naghama ya nyimbo.
Watu wengi haswa ma beachboy pia wanaongea Kiingereza, Kifaransa, Kitaliano, Kijerumani, Kiarabu, Kihispania, Kituruki, Kihindi n.k. kwa sababu za ugeni na utalii.
Utenzi maarufu sana huu. Ukipita pale tuki(tataki) utakutana nao kwa maprof wakiswahiliUTENDI WA MWANAKUPONA:
Mwenye kutunga nudhumu
Ni gharibu mwenye hamu
Na ubora wa ithimu
Rabbi tamghufiria
Ina lake mufahamu
Ni mtaraji karimu
Mwana Kupona Mshamu
Pate alikozaliwa
Tarikhiye kwa yakini
Ni alifu wa miyateni
Hamsa wa sabini
The author of this work
is a sorrowful widow
her worst sin
The Lord will forgive
Know her name
she is Reliant-of-the-Provider
Mwana Kupona Mshamu
born in Pate.
The date in reality
Is one thousand two hundred
Seventy-five.
--------
Mwana Kupona binti Msham (born on Pate Island, died c.1865) was a Swahili poet of the 19th century, author of a poem called Utendi wa Mwana Kupona ("The Book of Mwana Kupona"), which is one of the most well-known works of early Swahili literature.
Relatively little is known about her life. Her grandson Muhammed bin Abdalla [1] reported in the 1930s that Mwana Kupona was born on Pate Island, LAMU and that she was the last wife of sheikh Bwana Mataka, ruler of Siu (or Siyu), with whom she had two children. Mataka died in 1856; two years later, Mwana Kupona wrote her famous poem, dedicated to her 14-year-old daughter Mwana Heshima. Mwana Kupona died around 1865 of uterine hemorrhaging.
Utendi wa Mwana Kupona[edit]
The poem dates to about 1858 (year 1275 of the Islamic calendar), and is centered on the teachings and advice of Mwana Kupona to her daughter, concerning marriage and wifely duties.[2] Despite the seemingly secular subject, the book is prominently religious and even mystical, and it has been compared to the Biblical Book of Proverbs. A few lines of the poem are dedicated to the author herself:
Ukanimara mzee, adigo mara kukohiko mijikenda machiingira tanzania, nkweli asiliyehu yalakuko kwa arume amazu akaurika kayamba