Karibu Mwekezaji Kwaheri Uhuru

Karibu Mwekezaji Kwaheri Uhuru

Lidafo

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2019
Posts
889
Reaction score
1,789
Tanzania imekuwa ikipitia vipindi tofauti tofauti vya maswala makubwa ya kitaifa yanayohusu ushirikishwaji wa wanachi moja kwa moja, Suala linalotikisa kwa sasa ni suala la mkataba kati ya serikali yetu na kampuni ya DP world jambo hili linazidi kuchukua sura tofauti kila iitwapo leo kwani limefika hatua ya kubeba hisia za muungano, Udini na Ukanda.

Kwanza tujiulize ni kwanini suala hili limepokewa na jamii kwa ukubwa huu?

kiongozi yeyote na serikali kwa ujumla ni lazima ifahamu kuwa wanachi wanahitaji vitu vitatu tu, Ambavyo ni pesa, Chakula na amani. Kiongozi yoyote atakaye wapa wananchi vitu hivyo basi asiwe na wasiwasi hata asipopiga kampeni katika uchaguzi atachaguliwa tu tena kwa kishindo.

Sasa ukigusa mambo haya matatu wananchi ni lazima wapaze sauti na hapa hawawezi kuvumilia, Suala la bandari linagusa pesa, Chakula na amani ya watanzania hivyo kwa nia nzuri serikali inapaswa kusikiliiza maoni ya wananchi na kurekebisha pale penye mapungufu, Tukumbuke kuwa uwekezaji ni jambo nzuri kwa maendeleo ya taifa ila unatakiwa kuwa uwekezaji wenye tija.

Vifungu vya mikataba vimefafanuliwa na wanasheria mbalimbali, Wachambuzi na wabobezi wa maswala ya siasa hivyo sioni haja ya kuvirudia hapa. Ni wazi kuwa kwa aina hii ya mkataba tumemkaribisha mwekezaji tupate faida kwa maendeleo ya nchi yetu, Lakini wakati tunamkaribisha mwekezaji tuseme kwaheri uhuru wetu wa kupanga kuamua na kusimamia vya kwetu.
 
Watu wameshadadi bandari wakati kuna Taasis kibao zilishapokonywa majukumu na kupewa private 😅😅...Na list ni mnaona bandari tu.

Kabla ya kufa mzee Magu lissu alikuwa anaropoka eti serikali haifanyi biashara kabisa wapewe private kwa vile baadhi ya makampuni yana hisa zao hao CHADEMA.

Suala limeenda mpaka kweny bandari kaeni kwa kutulia sasa umbea umewaponza.
 
Watu wameshadadi bandari wakati kuna Taasis kibao zilishapokonywa majukumu na kupewa private 😅😅...Na list ni mnaona bandari tu.

Kabla ya kufa mzee Magu lissu alikuwa anaropoka eti serikali haifanyi biashara kabisa wapewe private kwa vile baadhi ya makampuni yana hisa zao hao CHADEMA.

Suala limeenda mpaka kweny bandari kaeni kwa kutulia sasa umbea umewaponza.
Hakuna mtu hataki uwekezaji kwenye bandari shida ni baadhi ya vifungu vinampa mamlaka makubwa DPW kuliko serikali
 
Back
Top Bottom