Karibu sana katika ziara yetu ya mafunzo ya kilimo na ufugaji nchini Kenya!

Habar mkuu,
Hii safari ni muhimu sana kwa wakulima wetu kwani kuna vitu vingi sana vya kujifunza kwa wenzetu pamoja na kwamba wao hawana ardhi kubwa ya kulima kama sisi lakin uzalishaji wao ni mkubwa sana.

Jambo la pili sijui wew nafasi yako ni ipi kwa hapo Tanzania ila kama una nafasi ya kuonana na watendaji wa serikali kwa maana ya wazir au watendaji wa wizara ya kilimo jaribu kuwashauri watenge nchi katika kanda na waweke mikakati ya kilimo kupitia hizo kanda kwa maana ya kwamba kuwe na vituo vya kutoa elimu kwa wakulima kulingana na kila kanda na aina ya mazao yanayolimwa kwenye kanda hiyo na pia angalau kila kanda iwe na maabara kwa ajili ya kupima ardhi na kuona inafaa kwa kilimo cha zao gani( wenzetu hapa Kenya wanafanya hivyo na wamefanikiwa pakubwa mkija mtakuja kuona).

Pia nimshukuru waziri wa kilimo ( Bashe ) ameanza kuwapa matumaini wakulima hata kuacha bei huru ya mazao amefanya jambo jema sana litakalowatia moyo wakulima kama unaweza kuwapata washauri watume wataalam wakafanye utafit wa masoko nnje ya nchi kwani mazao yetu ni ''hot cake'' huko nnje kama uingereza na kwingineko kwani bado tunalima kiasili ukilinganisha na watu wengine hii itasaidia kuunda vikundi au vyama kama hichi ambacho mnakuja kujifunza hapa kenya kwa maendeleo ya kilimo kwa watanzania.

Mwisho nashauri tangazo hili liwekwe kwenye vyombo vingi vya habari kadri itakavyowezekana kama magazeti, redio na ''social media'' ili liwafikie wengi zaidi mtanzania yoyote anaejihusha na kilimo na ufufagaji kwa namna yoyote namshauri asikose hii safari ni muhimu sana wazungu wanasema ''thank me later''.
 
Kwa uzoefu watu wengine wanapenda mafanikio ila hawako tayari kuyagaramia hayo mafanikio.
Na wao huamini mafanikio yanatoka kwa shetani ndiyo
maaana kila aliye fanikiwa humwita mchawi.
Nitakuwa mmoja wapo kama ratiba haita ingiliana na kazi yangu.
Asante
 
Kenya wako vizuri sana kwa kilimo na ufugaji na hata kuprocess mazao, nimependa kuprocess nuts, Tanzania bado kuna fursa kubwa ya kuprocess nuts kubwa Mno, Sema watu hawajaiangalia katika jicho lingine...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…