Karibu tufanye wote biashara ya kuagiza bidhaa ya Tomato Paste kutoka nje na kuuza nchini

JUMALIKA

Member
Joined
Dec 21, 2021
Posts
32
Reaction score
37
Habarini,

Kuna bidhaa ambayo inaitwa TOMATO PASTE hizi ni nyanya zilizochakatwa kiwandani na hutumika kama mbadala wa nyanya halisi. Kuna wakati hapa nchini kunakuwa na shida ya nyanya halisi kutoka mashambani na badala yake hizi nyanya ndio zinakuwa mbadala wake.

Zipo nyingi kutoka makampuni Mbalimbali kama hapa Tanzania RED GOLD anatengeneza ingawa Demand inakuwa kubwa mnoo kuliko Supply na husababisha ongezeko la Tomato zingine kutoka nchi za Misri na Oman na pengine tomato hizo ndio zinakuwa deal sana katika nchi yetu kama vile Almuzish kutoka Oman.

Mimi nilipata wadau ambao ndio walikuwa mabosi zangu na nikawa nafanya nao kazi kwa kusambaza hizo tomato zinaitwa KENZY TOMATO PASTE kutoka ughaibun kule Egypt. Ni biashara nzuri mnoo na tulipata soko zuri mnoo kwa bidhaa hii.

Ilifikia mahali demand ilikuwa kubwa kuliko supply na maboss wangu wakashindwa kuendana na speed ya wateja (mahitaji ya wateja), imefikia mahali sasa wameshindwa kuleta mzigo na biashara imesimama kwa muda mrefu sasa.

Naomba kwa mtu ambaye anaona kama tunaweza kufanya kazi basi mimi niko tayari tufanye kazi tukae chini na kufanya kazi maana Mtaji wa wateja mimi ninao na hadi leo hii mahusiano na hao wateja bado yapo vizuri zaidi.

Ni fursa nzuri mnoo, hii bidhaa japokua ina changamoto wakati ambao nyanya pori zinapatikana kwa wingi lakini ni sehem ya changamoto ya kila biashara, kwa anahitaji bidhaa hii ama kuhitaji ushauri wa kuingiza bidhaa nyinginezo kutoka nje basi mimi ndio master marketing wa yooote hayo; ninajua kuuza, ninajua Fast Moving product pia.

Mwenye utayari wa kuhitaji usimamizi wa biashara zake basi mimi nipo na sifa yangu kuu ni uaminifu na hofu ya mungu nikijaaliwa ubunifu. [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Uandishi mbovuu.. ahhh maneno yamebanana Sana kusoma yanaumiza macho mkuu
 
shida ni supply au mbona kila supermarket na corner shop zipo? Au shida ni bei na quality?

Wateja wako wanapenda brand gani kwa bei gani, sidhani kama uwepo wa nyanya fresh utazuia uuzaji wa hii ni different market segments ila uwepo wa hii kwa bei ya kutupa utapelekea wauza nyanya fresh soko lao kudumaa ilitokea Ghana na sisi itatokea baada ya mkataba na soko la ulaya
 
Nilikutumie ujumbe kwenye box yako ila huja jibu naomba unipigie ni juu ya tomato sauce
 
Namba yako kaka tafadhari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…