Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Wakuu,
Ukitembea tembea Duniani utagundua tabia za watu huendana na race yao. Mfano unakuta watu wa Afrika karibia wote tunataka kufanana tabia zetu isipokuwa watu wachache sana. Najua suala la tabia huweza kubadilika kutokana na factors mbalimbali, hivyo naimani kupitia uzi huu huenda tukabadilika kiasi flani.
Mie nitaanza kutaja tabia moja baada ya nyingine!
I) Sisi ni wavivu sana.
Yaani unakuta mtu anatamani kupata ajira ila hataki kazi. Yaani kuna ofisi nimewahi kufanya kazi, waajiriwa wengi hawapendi kabisa kazi. Wao wanapenda tu kupiga soga na wananuna wakipewa majukumu ya kufanya. Wanapenda zaidi kazi zenye posho posho. Ila posho isipokuwepo huoni kabisa morale yao... Hii ni tofauti na watu wa mataifa mengine.
ii) Sisi tunapenda sana connection ila tunalaumu viongozi wao wakipeana connection.
Unakuta mtu analaumu sana Viongozi wakipeana connection, ila yeye akipata fursa kidogo tu aanajaza watu wa familia/ndugu zake. Sasa kama na wewe unapenda connection unalaumu nini viongozi wakipeana connection. Hapa hoja ni kuwa sisi Waafrika tunaendekeza sana masuala ya kujuana na si uwezo wa mtu na kushindana kwa uwazi na uhuru.
iii) Sisi tunapenda sana mambo ya ushirikiana.
Aisee yaani unakuta watu wanakuambia wazi kabisa kuwa bila kwenda kwa Sangoma huwezi kutoboa kwenye kazi au biashara. Inashangaza sana.
iv) Tunapenda sana vyeo
Yaani unakuta mtu full kujipendekeza kwenye kazi utadhani anapenda kutimiza majukumu yake vizuri ila kumbe anajipendekeza kusaka cheo. Hatari sana aisee.
v)Hatujai kabisa masuala ya muda
Yaani mkipeana miadi ya kukutana muda flani watu hawajali kabisa muda
vi)Tunapenda sana ngono
Aisee, yaani mbaba/mkaka akimuona tu binti mzuri tayari ameshajijengea picha kuwa ampate vipi na afanye naye ngono. Yaani mwanamme akimuona msichana mzuri jambo la kwanza linalomjilia kichwani kwake ni ngono. Hatari sana hii.
vii) Viongozi wengi ni wabinafsi sana
Yaani mtu akipata nafasi yeye anachojua ni namna gani atapiga. Ni namna gani atajinufaisha kwa nafasi aliyonayo. Viongozi wengi ni matajiri ila ukifuatilia pesa walizonazo hazilingani na vipato vyao vya halali. Mjomba nii hivi mapesa yote, magari na majumba tutayaacha hapa hapa duniani.
viii) Watoa huduma wengi hawajali mambo ya customer care/satisfaction
Hapa sanasana ni watumishi wa umma. Yaani watumishi wengi hawajali kabisa mahusiano mazuri na wateja wao. Majibu yao na kuongea kwao kumejaa viburi na dharau ajabu kabisa.
ix) Ni wajanja janja sana na sii waaminifu
Aisee, ukilinganisha na watu wa mataifa mengine, kwetu sisi janja janja na kutokuwa waaminifu ndo tabia zetu. Yaani si rahisi kuaminika. Muafrika akikwambia jambo jifikirie mara mbili mbili. Hii ni tofauti kabisa na watu wa mataifa mengine kama Uchina, Korea, North Amerika na Ulaya.
List inaendelea na wewe unaweza kuongeza ya kwako...