Karibu tujadiliane uendeshaji mzima wa taasisi za kiraia (taasisi zisizo za kiserikali)

Karibu tujadiliane uendeshaji mzima wa taasisi za kiraia (taasisi zisizo za kiserikali)

yussufhajj

Member
Joined
Mar 24, 2016
Posts
27
Reaction score
8
Habari zenu wadau , kwa pamoja naomba tujadili uendeshaji mzima wa taasisi za kiraia
( jumuiya zisizo za kiserikali) . Hapa nataka tujifunze mambo mbali mbali kuhusu taasisi hizo na tupate uzoefu wa kuziendesha.

Kama upo katika taasisi fulani nataka utujuze miradi yenu , mafanikio na changamoto mnazo kabiliana nazo,

Kama hupo katika taasisi yoyote nahitaji maoni yako , ushauri au kama una wazo lolote la kutoa ambalo unahisi taasisi zikilitekeleza zitakwenda mbele,

Mwisho napenda kujitambulisha mm naitwa yussuf hajj mjumbe kamati tendaji kwaboko youth development association
( kwayda ).

"MITANDAO YA KIJAMII KWA AJILI YA MAENDELEO"
 
Okay. Issue za Donors ni changamoto sana lakini lazima muwe wabunifu katika fund raising, kupata external Donors kunahitaji commitments na jitihada za kutosha, lakini ili kufanya NGO isilale mnaweza kutumia local resources katika kuendelea kufanya community activities mfn.mnaweza mkaandika project proposal mkapeleka Vodacom, Tigo etc hili ni suala la kujaribu. Pia hao external Donors wakikuta NGO iko active inaleta taswira nzuri zaidi ya kuatract kutoa pesa. Kitu ambacho huwa tunakosea wakati wa kuanzisha NGO/CBO ni katika admission ya membership mfn; katika NGO/CBO mwenyekiti mnaweza kumchagua mtu ambaye ni influential eg. Professor, Politician, Musician, etc na pia members wengine lazima wawe asset kwa taasisi.
 
Pia katika uendeshaji wa taasisi za kijamii msijimilikishe sana ownership kwa sababu kuna kazi nyingine ambazo siyo kazima mpate fedha za Wazungu. Muanzishe utaratibu wa kudeploy volunteers katika maeneo ambayo mnafanya, muwapatie mafunzo wajue umuhimu wa kujitolea na nafasi yao katika jamii mfn; ukarabati wa barabara ya kijiji mnahitaji hela ya nini? Hapo kijijini hakuna watu wenye matoroli? Hakuna wenye majembe? Chepeo? Au kusafisha zahanati ya kijiji mnahitaji fedha? Please make effective use of your local resources available.
 
Back
Top Bottom