Karibuni Dar es Salaam wageni mnaokuja kutafuta maisha na kufanya biashara

Ila uwe tayari kupambana na vibaka magomeni mh!
 
CONTROLA nipo mkoani mambo hayenda kabisa ,nina miaka 23.

dzm napawaziaga sana ila weng wananiambia maisha ghali sana.

hapa nina million 1 cash,nikisema niuze na vitu vya getho inaweza fika million 1.3 nikija huko inaweza kunitoa au niendelee kuzichanga.


huku mishe haziend kabsa licha ya kupata icho kias.
 
Nyuzi zako zinanijengaga ubungo
 
Hii thread niliingoja kwa hamu sana Hii ni notice zungu nitazisoma mara kwa mara Mpaka nizimaster halafu niingie nazo Dar safari Hii nimeamua kuja na Nitakuja
 
bro simulia basi rafikiyo alivyosababish ulale selo
 
Dar watu wanafanya biashara za mitaji ya 30,000

Watu wanafanya Biashara za mitaji ya 50,000

Watu wanafanya biashara za mitaji ya 10,000

Hao wote kupitia biashara zao.kila mmoja wao jioni anarudi nyumbani kwake na chochote kitu.

Nimekupa mifano ya hao watatu uione kisha utajipima mwenyewe na huo mtaji wako ulio nao ukija utatoboa au lah...

Nadhani Dar inahitaji UTAYARI wako tu kuyatafuta maisha DAR hai hitaji capital (pesa)

Maana wapo/Tupo tulioanza from ZERO na sasa atleast tuna mudu 3 meals na tulikuja with nothing.

Jiulize swali 1, Nipo tayari kuyatafuta maisha? Kisha jibu lako litakuinua hapo ulipo sasa na kuanza kulifanyia kazi kwa vitendo.

Mil.1 usiifikirie sana tena usiiweke hata kwenye mahesabu Njooo akili yako ukiwa umeielekeza kwenye utafutaji na usiweke roho na macho yako kwenye hyo 1.3M

Maana unaweza Fika DAR tu leo Paaap Kwa mazingira ambayo hutoyajua wala kuelewa ukajikuta huna hiyo 1.3M una nguo ulizovaaa TU.

Usitake kujua zitaenda wapi, (huo ni mfano tu) inaweza isiwe kweli, sasa kama wakikwapua hizo hela Si utakuja dar uzimie ufe mkuuu?

Lakini kama akili yako uliiweka ktk kutafuta Utajisemea MIMI NI MTAFUTAJI 1.3M ni kitu gani? nimeshapoteza vingapi? utajiuliza maswali ya kijasiri kisha utaingia tena Mzigoni kutafuta pesa kama kijana mpambanaji.

Sishauri mgeni anaekuja DAR hata awe na mtaji wa 20M aanze biashara yyte, dar iko full of FAKE PEOPLE kila sehemu kila kona kila chobingo kila sehemu...

Kabla hujaanzisha biashara Dar kwa mgeni Kubali kuanza chini Jifanye mjinga Poteza hata mwaka mzima ukiusoma MJI na Watu wake.. Mwaka ni mrefu lkn utakuja siku 1 kujua umuhimu wa kusoma watu na mazingira ya eneo ulilopo.

Biashara inahitaji Research huwezi pata majibu sahihi ya utafiti unaoutaka dar kama utajitia umekuja ki don don una mipesa umeifcha bank.

Ili upate real info ni lazima ukubali kushuka ukubali kuanzia chini kule mchangani kwenye matope,kubali kudharaulika kidogo uje uheshimike Milele.

Dar inahitaji Akili si vinginevyo.
 
Mimi nikija dar nakuja na kodi ya miezi 3 na smartphone yangu na nauli ya mwendo kasi nimemaliza Mengine nitakutana nayo hukohuko

Uliwahi kuisikia story ya wale wapigana vita captain Wao alivyoichoma manuari yao baada ya kuvuka ng'ambo?

aliwaambia wanajeshi wake "Wote mmeona tumeichoma moto manuari yetu hatuna option nyingine zaidi ya kupigana na adui na kupata manuari zao ziturudishe nyumbani " FIKIRIA NINI KILITOKEA KWENYE UWANJA WA VITA
 
Hujaendeleza namna ulivyotusua
 
shukrani sana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…