Karibuni futari.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
KARIBU TUFUTURU



1)Jamvi natandika nje,njoni tukusanyane

Njoni goti tukunje,kwenye kheri tukutane

Hata kama ni vipunje,hivyo hivyo tugawane

Karibuni tufuturu,mwisho na dua tuombe.



2)Japo kidogo swadaka,ndugu njoo tujichane

Muda ule ukifika,ndugu zangu tukutane

Tuje kupata baraka,na kheri tuombeane

Karibuni tufuturu,mwisho na dua tuombe.


3)Jamani nawaalika,mawaidha twambiane

tule tukifurahika,na kheri tuelezane

Pamoja kukusanyika,tufurahi tusinune

Karibuni tufuturu,mwisho na dua tuombe.


SHAIRI-KARIBU TUFUTURU.

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha

+255624010160

iddyallyninga@gmail.com
 
Wakati nafungua huu uzi nlitegemea kukutana na mapichapicha picha ya maakuli ya futari,lahaula kumbe fasihi andishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…