Karibuni kuijaribu - Microsoft Excel translator add-in

Karibuni kuijaribu - Microsoft Excel translator add-in

herman3

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
556
Reaction score
736
Habarini wakuu
Nimewatengenezea MS Excel add-in ambayo inakusaidia kufanya translation, mfano kuna wakati unaweza kuwa na column ambayo ipo na rows nyingi ambazo content zake zipo kwa kiingereza na unataka kuzitafsiri kwenda kiswahili au lugha nyingine.

Si rahisi sana kufanya hivyo kwa kuandika row to row, lakini kwa kutumia add-in hii utafanikisha hilo kiurahisi kabisa kwa kuingiza formular hii:

=LUGHA("sw",A2) kisha bonyeza enter (Yaani LUGHA inawakilisha function, sw inawakilisha lugha unayotaka itokee, A2 inawakilisha cell unayotaka kuitafsiri) tazama picha hii.

1677503308878.png


Baada ya hapo bonyeza ENTER itakuletea hivi baada yapo utaweza drag hiyo function kwa cell nyingine zote na itakupa tafsiri ndani ya sekunde chache

1677503410406.png

Tumia short code za lugha kwenye function mfano
kiswahili =LUGHA("sw",A2)
English =LUGHA("en",A2)
Germany =LUGHA("de",A2)
Russian =LUGHA("ru",A2)
Vivyo hivyo kwa lugha nyinginezo

Unaweza download add-in hii kwa kubonyeza hapa https://cv.ajirasearch.com/Excel%20Translator%20Add-in%20-%20Helman.xlam
ZINGATIA: Add-in hii inatumia internet kuweza kufanya kazi.
Unaweza kuijaribu na kunipa feedback ili niweze kuboresha zaidi

Namna ya ku_install Add-In hii
  1. Hakikisha umeruhusu developer mode kwenye Excel yako. Kama hujaruhusu developer mode fanya hivi
    1. Bonyeza file
    2. Bonyeza Options
    3. Bonyeza Customize Ribbon
    4. Weka tick kwenye menu hizi Developer na Add-ins
    5. Baad ya hapo bonyeza OK
2. Baada ya hapo bonyeza Developer, kisha bonyeza Excel-Add-ins
3. Bonyeza Browse, kisha chagua add-in uliyodownload kisha bonyeza ok
4. Baada ya hapo weka alama ya tick kwenye add-in hii kisha bonyeza ok

Baada ya hapo ukibonyeza =LUGHA kwenye cell yoyote function hii itakuwa active na itaweza kufanya kazi vizuri kabisa.

Kama utakwama sehemu yoyote nitaweza kukusaidia bure kabisa.
 
Kizazi sana hii kitu xcel siijui lkn naipenda sana na nimekuja kugundua nusu ya maisha ya mwanadam anatumia xcel pasipo yeye kujua naomba nisaidie namna ya kuandaa kufunga hesabu za buashara ya miamala km tigo pesa kwa kutumia smartphone
 
Back
Top Bottom