Preta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 24,320
- 18,852
Wadau ningependa kuwakaribisha nyumbani siku hii ya leo. Najua kila mmoja ana furaha moyoni mwake hivyo basi nafikiri sijachelewa sana. Mbuzi ndo kashachinjwa, mbege inaendelea kunywewa taratibu, manyanga namuona pale anabadili santuri kaweka ya lucky dube, mawalla ndo kwanaza anafika kutoka kanisani misa ya kwanza, mambore na malyimo wanamenya ndizi, huyu mtui sijui kashalewa ngoja tumuache maana kaamkia kunywa ngera. direction ya eneo la tukio ni ukishafika marangu mtoni panda kidogo mpaka chuo cha ualimu opposite na chuo kuna njia inakula kushoto kama hatua kumi utajua umefika maana shamrashamra si za kipolepole, welcome sana mndenyi