Karibuni nyumbani

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
24,320
Reaction score
18,852
Wadau ningependa kuwakaribisha nyumbani siku hii ya leo. Najua kila mmoja ana furaha moyoni mwake hivyo basi nafikiri sijachelewa sana. Mbuzi ndo kashachinjwa, mbege inaendelea kunywewa taratibu, manyanga namuona pale anabadili santuri kaweka ya lucky dube, mawalla ndo kwanaza anafika kutoka kanisani misa ya kwanza, mambore na malyimo wanamenya ndizi, huyu mtui sijui kashalewa ngoja tumuache maana kaamkia kunywa ngera. direction ya eneo la tukio ni ukishafika marangu mtoni panda kidogo mpaka chuo cha ualimu opposite na chuo kuna njia inakula kushoto kama hatua kumi utajua umefika maana shamrashamra si za kipolepole, welcome sana mndenyi
 
Give the correct address, like numbers and names, my GPS doesn't understand when you say "nyumba iko chini ya mbuyu"

I can't wait kula kiamba.
 
direction ya eneo la tukio ni ukishafika marangu mtoni panda kidogo mpaka chuo cha ualimu opposite na chuo kuna njia inakula kushoto kama hatua kumi utajua umefika maana shamrashamra si za kipolepole, welcome sana mndenyi

Kama nishawahi kufika eneo hili.. Haufiki CAPRICON HOTEL?
 
Give the correct address, like numbers and names, my GPS doesn't understand when you say "nyumba iko chini ya mbuyu"

I can't wait kula kiamba.

Ndugu yangu KIU kwa swala la address kwa kweli utanisamehe, huku kwetu huwa tunafahamiana kijiji kizima so hatuna sababu ya kuweka na namba za nyumba au sijui wenyewe ndio mnaziita zip code sisi hatuna we ukifika karibu na hapo niliposema ni pm nitakuja kukuchukua
 
Mkuu naniliu nipo hapamarangu mtoni tayari hebu nipe maelekezo ya ziada...nasikia mpwa Xpin sauti iko juu au ameanzia kwa Mrema?
 
Mkuu naniliu nipo hapamarangu mtoni tayari hebu nipe maelekezo ya ziada...nasikia mpwa Xpin sauti iko juu au ameanzia kwa Mrema?

Sasa panda kidogo kwa juu kama unaenda chuo cha ualimu kuna gorofa leupe kushoto fata hiyo njia shuka nayo, Xpini nilimuona jana pale kwa Kelewa kakaa kaunta, kwa kweli xmas haikuwa mbaya kwa nini hukuja jana lakini?
 
Maaaaaaaaan!, we need house planning!, shuka, panda mpaka saa ngapi?
 
Maaaaaaaaan!, we need house planning!, shuka, panda mpaka saa ngapi?

Inaelekea wewe sio mwenyeji hapa nchini i mini tanzania, umeona kijiji gani kina house planning, nahisi kenu ni gezaulole
 
Inaelekea wewe sio mwenyeji hapa nchini i mini tanzania, umeona kijiji gani kina house planning, nahisi kenu ni gezaulole

May be we can start now...how bout that?
 
Mkuu nilichelewa hii post ningekuja kula mbuzi na maji makubwa. Vipi andaa ya mwaka mpya basi bosi
 
Mkuu nilichelewa hii post ningekuja kula mbuzi na maji makubwa. Vipi andaa ya mwaka mpya basi bosi

usijali mwaka mpya tunaangusha ngombe kabisa ila nitawajulisha yanayojiri na nafikiria kubadili venue ila nitawataarifu wale wote wanaotaka kujumuika na mimi
 
usijali mwaka mpya tunaangusha ngombe kabisa ila nitawajulisha yanayojiri na nafikiria kubadili venue ila nitawataarifu wale wote wanaotaka kujumuika na mimi
Mkuu fanya hili jambo serious bana tuje tunywe mtori, nasubiri kwa hamu ukaribisho huu wa sasa sintoukosa
 
ninachofanya kwa sasa ninachukua idadi yenu kwa wale watakaokuja ili niweze kuandaa eneo la kutosha kujimwayamwaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…