Karibuni zanzibar

ALNASHIR

New Member
Joined
Sep 6, 2013
Posts
4
Reaction score
2
ROSE NA ALNASHIR NI WAZALIWA WA NACHINGWEA NA TABORA, TUME FUNGUA HOTEL (BED & BREAKFAST) ,"THE ROSAL STONE TOWN HOTEL" MAENEYO YA KOKONI, HOUSE NA 1226 STONE TOWN ZANZBAR,NI DAKIKA MOJA KUTOKA DARAJANI, UKIFIKA PEOPLES BANK OF ZANZIBAR INGIA KWENYE KICHOCHORO, UMESHAFIKA, PIA NI DAKIKA NNE KUTOKA GATI YA FERRY. NI KARIBU NA SEHEMU ZOTE ZA KITALI STONETOWN, NA HOTEL NA BAR ZOTE STONETOWN.
MARA NYINGI WABONGO WAKIFIKA ZANZIBAR WANAJISIKIA KAMA WAGENI, KARIBUNI KWETU, SISI NI WA BONGO PIA NA TUTAWA SAIDIYA KUPATA HUDUMA TOFOATI ZA HAKIKA, NA KWA BEI NAFUU, DOLFIN SAFARIS, SPICE TOURS, STONE TOWN TOURS, KUPOKELEWA NA KURUDISHA AIRPORT AU KWENYE GATI LA FERRY, KARIBUNI KWETU MJISIKIE NYUMBANI.
KARIBU SANA
ROSE NA ALNASHIR
TEL +255752850400 ALNASHIR, +255765939393
FACEBOOK/ROSAL STONETOWN HOTEL
www.therosalstonetownhotel.com
rosalhotel@yahoo.com
akassamali2000@yahoo.com
 

Attachments

  • securedownload[6].jpg
    82.3 KB · Views: 117
  • IMG_3647.jpg
    20.4 KB · Views: 99
  • IMG_3653.jpg
    17.8 KB · Views: 91
  • IMG_3664.jpg
    18.3 KB · Views: 85
Asante. Bei za vyumba zipoje mkuu. Na vipi kama nakuja na mpenzi wangu, ni lazima kuwa na cheti cha ndoa? Bia zipo?Nitarudi
 
You should put the pricing then, what exactly do you offer/ differ from the other hotels, msije sema n Hotel kumbe is just Guest house. More information please + packages
 
Kwanza nahofia usalama,kwani jamaa zetu wakijua hiyo hotel ni ya wabara kuna siku itrushiwa bomu la petrol au wageni kuvamiwa na kumwagiwa tindikali,umefanya kosa kutangaza kuwa mnaomiliki hiyo hotel ni wabara,pia umesema wabara karibuni sana humu JF wapo washabikia Uzanzibar kujitenga na hao ndio wataenda huko maskani kutangaza kuwa hotel flni ni chocholo la wabongo,Pia weka na bei na jibu maswali ,
 
Usiwe na Hofu, Uki ishi na watu vizuri, wataku pokea na upendo, Ndivyo na siis tuna husiano nzuri na jamii na majirani, na wageni wano fika siyo lazima ni wa bongo tuu bali wageni wa kila aina wana kairibishwa.Karibu Sana, Alnashir
 
Asante sana Bi. Rose na Bw. Alnashir kwa mawaliko wenu. Nimefurahi sana kukuta post yenu katika Jamii Forum. Kama mtakumbuka, nilishawahi kufika katika hoteli yenu na nililala hapo siku mbili. Katika holidays zangu zote, sehemu niliyokaa na kujihisi niko nyumbani ni katika hoteli yenu kwani mlinikarimu vizuri sana. Bado nawashukuru sana kwa msaada wenu mkubwa mlionipa katika kuandaa spice tour na dolphin safari. Hoteli yenu pia ni safi sana na vyumba vyake vina hadhi ya juu mno. Bei zenu pia ni nafuu sana kilinganisha na hoteli zipatikanazo Stone town. Lazima nikiri kwamba milo ya asubuhi (Breakfast) niliyopata hapo kwenu ulikuwa ni mzito na yenye ubora. Pia, wafanyakazi wenu ni wakarim, wacheshi na wamebobea katika kazi yao. Sitosita kuwashawishi ndugu, jamaa na marafiki kufikia hapo kwenu mara watakapo kitembelea kisiwa cha Unguja hapo Zanzibar-Stone town. Ni mimi, Steve Robert (Kutoka Dar-es-salaam).
 
nani aje huko amwagiwe tindikali? kaeni peke yenu. hata watalii mtakuwa hampati sijui mtakula nini. nusu yenu mtageuka ombaomba na mabwabwa
 
Bei zime tangazwa kwenye kipeperushi, Siyo Lazima uje na cheti cha ndoa au ya kuzaliwa, Uje na Kitambulisho itahitajiwa bandarini, Bia hamna lakini kuna bar na sehemu za chakula nyingi kila cona Zanzibar, Karibu sana
 

For Promotional Use or Multipile ID only.
 
Ingekuwa ni vyema ukaweka na bei kabisa mkuu for booking purposes..Mtu anatakiwa kufanya decision na kujuwa kama vi perdiem vyangu navyolipwa hapa vinakidhi haja kuishi hapo......Hakuna kitu kinachoniboa Zanzibar kama bei za Hoteli amabzo zimekuwa haziendani na uhalisia...ni ghali mno. Pia kujitambulisha kuwa mnatoka bara watch out uamsho wasiwaamkie...
 
Ningependa kuwafahamisheni nyote kuwa Hoteli hii ya Rosal ipo kati sehemu yenye usalama wakutosha katika kitovu cha mji mkongwe huo wa Zanzibar. Ni muhimu kujua kwamba si mara yangu ya kwanza kufika Zanzibar kwani nilishakaa kwa muda wa miaka miwili huko Zanzibar kikazi. Kwa mtazamo wangu, wazanzibari kwa ujumla ni wakarim na hawana matatizo na watu wa bara na hata watalii wa kimataifa ingawa kuna baadhi ya watu wanaouchafulia sifa nzuri uma huo. Katika mda wote niliakaa huko, nilipata marafiki wengi ambao bado ninamahusiano mazuri nao. Pia sikuwahi kupata bugdha yoyote ile kutoka kwa Mzanzibari hata mmoja. Nilivyofika Zanzibar mara hii (siku chache zilizopita), nilikuta watalii wengi sana kutoka nchii mbali mbali na walikuwa wakitembea mitaani bila hofu yoyote. Nikipata nafasi nyingine ya kwenda Zanzibar, nitaitumia ipasavyo bila kusita hata kidogo, na ningependa kuwaondoa hofu watanzania wenzangu kuhusu hali ya usalama hapo Zanzibar.
 
Asante. Bei za vyumba zipoje mkuu. Na vipi kama nakuja na mpenzi wangu, ni lazima kuwa na cheti cha ndoa? Bia zipo?Nitarudi
MOST wellcome !! haswa wewee tunakusubiri bila malipo (buree) wewe ni mteja adimu !!
 
Vp,nafasi Za Kazi?nna Dogo Wangu Kasomea Mambo Ya Hotel Management
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…