Karikakoo Festival kufanyika August 24-31, 2024 viwanja vya Mnazi Mmoja, bidhaa kuuzwa bei ya punguzo

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
IMG_4971.jpeg

Jumuiya ya wafanyabiashara Kariakoo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanatarajia kufanya tamasha walilolipa jina la 'Kariakoo Festival ' kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia tamasha hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Karikakoo, Martin Mbwana amesema kuwa wanatarajia lifanyike kwa wiki nzima kuanzia August 24-31, 2024, kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali katika eneo hilo na kuuza vitu kwa bei nafuu.

"Idadi ya wafanyabiashara Karikakoo ni elfu 35 hadi elfu 40, tunategemea kwa kuanza tuwe na wafanyabiashara elfu 15 hadi elfu 20"amesema Martin

Amesema kuwa kupitia tamasha hilo wafanyabiashara wa Kariakoo watapata fursa ya kusafisha stoo zao kwa kuwauzia wateja kwa bei rafiki.

Ameongeza kuwa wanatarajia kutumia fursa hiyo kujitangaza sambamba na kujuana huku pia akidai kuwa wananchi watanufaika na huduma zitakazokuwa zikitolewa.

Hata hivyo amebainisha kuwa wameandaa utaratibu wa Wafanyabiashara kujiandikisha mapema ili waweze kuwaandalia utaratibu rafiki katika eneo husika ambapo tamasha linatarajiwa kufanyika, hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza.

IMG_5134.jpeg

Pia waratibu wa tamasha hilo wameeleza kuwa dhamira kuu ni kukuza soko kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wateja huku pia tija wanayotarajia kupatikana ni pamoja wafanyabiashara kutanua wigo wa soko la ndani na nje kwa kuwa matarajio yao ni kuwa kutakuwepo na watu kutoka mataifa mbalimbali.

Lakini pia imeongezwa kuwa katika tamasha hilo, kutakuwepo pia na bidhaa za viwandani pamoja na bidhaa zinazoweza kutumika kama nishati mbadala ya kupikia.

Aidha imeelezwa kuwa tamasha hilo litaenda sambamba na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa ndani na nje.
 
Hao uongozi wanataka kukusanya pesa za viingilio za wafanya biashara tu hapo mnazi mmoja hapawezi kuaccomodate wafanya biashara elfu15 huo ni uongo! Waache janja janja maana hapo wataojaa ni machinga wataopewa bidhaa na matajiri na ambao hawatoi risiti.
 
Jumuiya ya wafanyabiashara Kariakoo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanatarajia kufanya tamasha walilolipa jina la 'Kariakoo Festival ' kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia tamasha hilo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Karikakoo, Martin Mbwana amesema kuwa wanatarajia lifanyike kwa wiki nzima kuanzia August 24-31, 2024, kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali katika eneo hilo na kuuza vitu kwa bei nafuu.

"Idadi ya wafanyabiashara Karikakoo ni elfu 35 hadi elfu 40, tunategemea kwa kuanza tuwe na wafanyabiashara elfu 15 hadi elfu 20"amesema Martin

Amesema kuwa kupitia tamasha hilo wafanyabiashara wa Kariakoo watapata fursa ya kusafisha stoo zao kwa kuwauzia wateja kwa bei rafiki.

Ameongeza kuwa wanatarajia kutumia fursa hiyo kujitangaza sambamba na kujuana huku pia akidai kuwa wananchi watanufaika na huduma zitakazokuwa zikitolewa.

Hata hivyo amebainisha kuwa wameandaa utaratibu wa Wafanyabiashara kujiandikisha mapema ili waweze kuwaandalia utaratibu rafiki katika eneo husika ambapo tamasha linatarajiwa kufanyika, hivyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza.

Pia waratibu wa tamasha hilo wameeleza kuwa dhamira kuu ni kukuza soko kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wateja huku pia tija wanayotarajia kupatikana ni pamoja wafanyabiashara kutanua wigo wa soko la ndani na nje kwa kuwa matarajio yao ni kuwa kutakuwepo na watu kutoka mataifa mbalimbali.

Lakini pia imeongezwa kuwa katika tamasha hilo, kutakuwepo pia na bidhaa za viwandani pamoja na bidhaa zinazoweza kutumika kama nishati mbadala ya kupikia.

Aidha imeelezwa kuwa tamasha hilo litaenda sambamba na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa ndani na nje.
Kidumu Chama cha Mapinduzi
 
Back
Top Bottom