Karim Mandonga alivyopokelewa kwenye ofisi za Balozi wa Tanzania Nchini Kenya

Karim Mandonga alivyopokelewa kwenye ofisi za Balozi wa Tanzania Nchini Kenya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. John Simbachawene amekutana na bondia Mtanzania Karim Mandonga na kumpongeza kwa ushindi wake dhidi ya bondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi katika pambano lililofanyika Jumamosi nchini Kenya.

Mand.jpg

Mando.jpg

Mandonga.jpg

Mandon.jpg
 
Kimasikhara tu jamaa anazidi kuchanja mbuga huku aliemtandika( kaoneka) akichanja Kuni. Leo kakabidhiwa gari huku jamaa aliempa umaarufu amepotea kabisa hata Kwenye ulimwengu wa ngumi. Aliepigwa kapata deal uingereza wakati akina mfaume mfaume na kiduku wapambanaji halisi hawajulikani wanachokifanya.
 
Hiyo ndio heshima ya nchi ,ukiwa balozi ugenini halafu unatembelewa na vijana wanaoipa heshima nchi yako inapandisha hadhi nchi. Sio wale wabanapua wanaovaa mahereni kama wanawake na kujichora tattoo za Hina kuwaiga wazungu au yule mwehu aliyesoma kapoteza viatu airport
 
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. John Simbachawene amekutana na bondia Mtanzania Karim Mandonga na kumpongeza kwa ushindi wake dhidi ya bondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi katika pambano lililofanyika Jumamosi nchini Kenya.
Ubalozi wa nchi yako ugenini ni kama nyumbani, so sio ishu. Ingekuwa na uzito kidogo kama angepokelewa kwenye ubalozi wa Canada nchini Kenya
 
Kimasikhara tu jamaa anazidi kuchanja mbuga huku aliemtandika( kaoneka) akichanja Kuni. Leo kakabidhiwa gari huku jamaa aliempa umaarufu amepotea kabisa hata Kwenye ulimwengu wa ngumi. Aliepigwa kapata deal uingereza wakati akina mfaume mfaume na kiduku wapambanaji halisi hawajulikani wanachokifanya.
Dunia na asili vina utaratibu wake aliyejaliwa ndo anapata.
 
Sahihi kabisa.

Mandonga kajua kujibrand sana.

Hivi zamani alikuwa anapigana wapi? mbona kaibuka juzi kati hapa

Atakua alikuwa anacheza mapambano ya mtaani tu (ameture fighting) ila jina lake pamoja, mazoezi na mikwara yake ndio iliompa chati zaidi, nae anakwenda na upepo huo.

Cha muhimu kwake awe makini kwa kuwekeza katika kipindi hiki nyota yake inapong'aa,

"Asisindikize watu katika Utajiri"
by Salam SK
 
Back
Top Bottom