Karl Marx on The Bourgeoisie & Proletariat: MABWENYEYE VS WALALAHOI

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
HAPA NDIPO TULIPOFIKA KWA SASA

Simply put, the bourgeoisie is the oppressive class, which Karl Marx argued would be destroyed in the workers' revolution. Specifically, the bourgeoisie was the class which controlled the means of production as well as almost all of the wealth.

In Swahili, the term "bourgeoisie" can be translated as "tabaka la mabwanyenye" or "mabwanyenye". The adjective form, "bourgeois," can be rendered as "kibwanyenye".

The term "bourgeoisie" refers to the social class that owns the means of production and controls capital, often associated with the middle or upper-middle class. In Marxist theory, it is the ruling class under capitalism.
 
Umemaliza kuandika au hii ni Part 1 ?
 
23 November 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini Tanzania


View: https://m.youtube.com/watch?v=1MRrHjRF5ZQambao walikuwa Brazil kushiriki mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali zenye Uchumi Mkubwa zaidi duniani (G20 SSummit 2024) mara baada ya kukamilika kwa Mkutano huo, Rio de Janeiro ,nchini Brazil tarehe 19 Novemba ,2024
 

11 August 2025​

Mkutano na Waandishi wa Habari, CCM Lumumba​



View: https://m.youtube.com/watch?v=Q6DYmzJ08QA
Mkutano wa Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo vya Habari na Ndg. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, Tanzania
 
12 August 2025
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA CCM MHE. RAIS DKT. SAMIA AKISHIRIKI CCM 2025 GALA DINNER...


View: https://m.youtube.com/watch?v=RP0DpdgSjVsLeo nimepata nafasi ya kuhudhuria CCM GALA DINNER 2025 kutunisha fuko la fedha la chama dola kongwe tawala kwa ajili ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2025

Chairperson of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) and President of the United Republic of Tanzania, Dr Samia Suluhu Hassan, today, August 12, 2025, arrived at Mlimani City in Dar es Salaam to attend the CCM 2025 Gala Dinner.

The high-profile event is aimed at raising funds to support the party’s campaign activities ahead of the October 29 General Election. The fundraising dinner brings together party leaders, members, supporters, business stakeholders, and well-wishers from across the country.

According to party officials, proceeds from the event will be used to coordinate nationwide campaign programs, including public rallies, media engagements, and grassroots mobilization in preparation for the polls.

Dr Samia’s presence at the event underscores CCM’s commitment to mobilizing resources early to ensure a well-organized and impactful campaign period



View: https://m.youtube.com/shorts/ij79VuB413c

View: https://m.youtube.com/shorts/yL_7Y5ZLsvg
 
Tujadili muunganiko wa mabepari uchwara na matajiri wote kutiki October 2025 ina maana gani kwa musktakhabali wa taifa leo.

Wahariri waandishi wa habari, matajiri, viongozi wa klabu kubwa za soka, influencers, celebrities, media zote za habari kuripoti chama kimoja kongwe dola usiku na mchana 24/7 n.k

Muunganiko huu una afya gani kwa demokrasia ya taifa leo ?

Toka maktaba :

UmkhontoweSizwe​

Wasomi wetu ni hopeless tu kama wanasiasa, hawana tofauti. Makundi haya mawili wameungana pamoja kuunda kundi la "Bourgeois" wasiojali walio chini yao kwa lengo la kulinda maslahi yao binafsi waliyojipatia kwa njia zisizo halali. Sisi makapuku need to fight back​

 
Rais Javier Milei wa Argentina atoa hotuba murua na kutoa tahadhari ya Hatari ya kuongezeka kwa mawazo ya chama cha kijamaa, hatamu za kiuchumi kushikiliwa na serikali

View: https://m.youtube.com/watch?v=cjONc43KsEo Uhuru na Maendeleo ya Watu! (Makofi)! Kwanza kabisa, nashukuru sana kwa mwaliko huu. Kuhusu mkutano wa leo na athari zake, hapo awali nilizungumza huko Davos ambapo nilisisitiza. hatari ambayo nchi za Magharibi (na hata Tanzania) inakabiliana nazo kutokana na kuongezeka kwa mawazo ya kijamaa, nguzo na hatamu za kiuchumi kushikiliwa na serikali. Leo, nitaangazia misingi ya kiufundi ambayo ilisimamia mitazamo ya kisiasa niliyoshiriki katika mkutano huo.

Nitajadili jinsi uchumi wa mamboleo na mtazamo wake juu ya kufeli kwa soko unavyowezesha mawaza ya kiujamaa, hatimaye kukwamisha ukuaji wa uchumi na mapambano dhidi ya umaskini.


Kiini cha suala hili kiko katika mgongano wa kimbinu kati ya modeli ya mawazo ya kinadharia na matukio yanayotokea ulimwengu katika uhalisia.

Kwa ujumla, modeli inaposhindwa kuendana na hali halisi, tunarekebisha au kutupa kielelezo cha modeli. Hata hivyo, katika mfumo wa uchumi mamboleo, kunapokuwa na tofauti, huwa wanalaumu 'ukweli' kwa kusababisha 'kufeli kwa soko.'

Hii inatokana na kukaririshwa somo la uchumi tulilosoma vyuoni kuhusu mizania ya vipengele vya kawaida vya usawa wa ushindani - uwepo bidhaa , upekee wa bidhaa , na kila kitu kuwa sawa yaani utulivu.

Tatizo linatokea kwa uchambuzi wa kawaida kupitia uchambuzi wa fomula ya Pareto. Kwamba Ubora wa formula ya mizania ya Pareto unapendekeza kuwa kuboresha hali ya mtu bila kuzidisha hali ya mwingine ni uboreshaji wa Pareto.

Fursa hizi zinapoisha, tunafikia kiwango bora cha Pareto, na hivyo kusababisha ufafanuzi wa 'kufeli kwa soko' - ushirika usio leta mabadiliko, athari za kutoka nje, bidhaa za umma, tofauti za taarifa , na ile hali inayoitwa Wafungwa kulaumiana kwa sababu ya kutopeana ushirikiano. Fasiri hizi zote huwezesha ushawishi wa uingiliaji kati wa serikali na kuendekeza ajenda za serikali kushika nguzo za kiuchumi na ujamaa


Ili kufafanua hili kwa lugha nyepesi , fikiria enzi za mpito karne ya miaka ya 1800 kutoka kutumia mishumaa hadi balbu za taa ya umeme ili tupate mwanga. Ikiwa serikali husika miaka hiyo wangefuata njia ya kuingilia kati kuokoa viwanda vya uzalishaji mishumaa kufilisika pia ajira kupotea, basi leo hii mwaka 2024 bado tungekuwa tunatumia mishumaa badala ya kufurahia mwanga wa kisasa wa balbu za umeme.

Hivi ndivyo ujamaa unavyoweza kuathiri maisha yetu. Tunahitaji kusonga mbele zaidi ya kiwango bora cha Pareto kinachoamini katika mizania ya usawa, na kukumbatia maendeleo.

Soko liangaliwe kama ni mchakato wa ushirikiano wa kijamii ambapo haki za mali hubadilishwa kwa hiari. Kwa kuwa ubadilishanaji ni wa hiari, dhana ya 'kushindwa kwa soko' / market failrure inakuwa haina maana.

Misingi ya soko ni pamoja na mali ya kibinafsi na uingiliaji mdogo wa serikali. Mfumo wa bei, unaotokana na ubadilishanaji huu, hufanya kazi kama kisambaza habari na utaratibu wa kuratibu.

Mali ya kibinafsi na soko huria hurahisisha hesabu za kiuchumi, kufichua uwezekano wa ujamaa. Ujamaa unakosa mali binafsi na taratibu za soko, hivyo kusababisha uzembe na upotoshaji.

Ushindani, si kwa maana ya kisasa ya ushindani kamili, lakini kama kuingia na kutoka bila malipo, ni muhimu.

Dhana ya mchumi nguli Adam Smith ya mgawanyo wa kazi na ushirikiano wa kijamii inasisitiza kutofaulu kwa mawazo ya ujamaa. Smith alionyesha jinsi kazi maalum huongeza tija kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, bila mahitaji, mgawanyiko wa kazi hauwezi kutekelezwa kikamilifu. Licha ya tofauti zozote za kibinafsi, washiriki wa soko lazima washirikiane, kukuza amani na kudhoofisha ujamaa.

Wafanyabiashara waliofaulu katika mfumo wa kibepari hunufaisha jamii kwa kutoa bidhaa bora kwa bei bora, kuunda nafasi za kazi, na kukuza maendeleo. Wajasiriamali ndio nguzo ya mafanikio.

Sasa, hebu tushughulikie mtanziko wa uchumi mamboleo ndani ya nadharia ya ukuaji wa uchumi. Takwimu za kihistoria zinaonyesha kuwa kutoka enzi ya Ukristo hadi 1800, Pato la Taifa kwa kila mtu libaki bila kukua .

Walakini, kuanzia miaka ya 1800 na kuendelea, iliongezeka zaidi ya mara 15, na idadi ya watu ulimwenguni iliongezeka kutoka milioni 800 hadi bilioni 10. Kipindi hiki pia kilishuhudia kupungua kwa umaskini uliokithiri, kutoka 99% hadi 5%.

Nadharia ya za kiuchumi mamboleo yaani Neoclassical inakosoa ukiritimba, lakini kipindi hiki cha miundo ya ukiritimba kilileta ustawi mkubwa na kupunguza umaskini.

Uchambuzi wa wana uchumi mamboleo una dosari kwa sababu hurahisisha kupita kiasi na kushindwa kuzingatia athari za siku zijazo na uchumi mzima.
Ukiritimba, kulingana na nadharia ya neoclassical, huzalisha kidogo na malipo zaidi.

Walakini, faida ya ukiritimba inaweza kuchochea matumizi, uzalishaji, na ajira katika sekta zingine. Kuokoa faida hizi husababisha uwekezaji na ukuaji.

Hata kama ukiritimba anajilimbikizia mali, hupunguza usambazaji wa pesa, kupunguza bei na kunufaisha idadi ya watu.
Uingiliaji kati wa serikali kwa jina la haki ya kijamii, demokrasia isiyo na kikomo, na kujitafutia umaarufu yaani populism mara nyingi hudhuru uchumi.

Nchi kama vile Argentina, zilizowahi kuwa miongoni mwa nchi tajiri zaidi duniani, zimeanguka kwa kiasi kikubwa kutokana na miongozo/ kanuni nyingi na kuingiliwa na serikali.

Ubepari, kinyume na shutuma za ubinafsi wa kupindukia, sio tu kwamba una tija zaidi bali pia ni wa haki. Soko, kama mchakato wa ugunduzi, hutengeneza utajiri wakati wa uzalishaji. Wale wanaogundua au kuunda thamani mpya wanaimiliki kwa njia halali ...



NeoClassical theory The Pareto Principle is very simple, yet very important. It is named after Italian economist Vilfredo Pareto, who, in 1906, found that 80% of the land in Italy was owned by 20% of the population.

What was most important about Pareto’s finding was that this 80/20 distribution occurs extremely frequently. For example, in general, 20% of your customers represent 80% of your sales. And 20% of your time produces 80% of your results. And so on
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…