Karl Peters - baba wa taifa kihalisi?

Mwanamkiwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
2,023
Reaction score
2,402

Katika Tanzania tumezoea kusema Mwalimu Julius Nyerere ndiye Baba wa Taifa. Hii ni kweli kwa kwa taifa la kisasa la Tanzania. Maana Nyerere pamoja na Abeid Amani Karume wa Zanzibar waliamua kuunganisha nchi za Tanganyika na Zanzibar kuwa nchi moja.

Ila tu Mwalimu Nyerere aliwahi kuwa kiongozi wa Tanganyika. Hakuanzisha Tanganyika. Aliirithi tu kutoka Mwingereza.
Lakini ni nani aliyeanzisha Tanganyika?
Kihistoria kuna majibu mawili:
A) Serikali ya Uingereza iliamua kuchukua koloni ya awali ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (baada ya kushinda Ujerumani 1918), Kuachia Ubelgiji sehemu ndogo za Burundi na Rwanda, na kuita yote "Tanganyika"

ila tu kihistoria kuna jibu la kiundani zaidi:
B) mnamo mwaka 1884 kijana Mjerumani kwa jina la Karl Peters aliamua kutafuta koloni kwa Ujerumani katika Afrika ya Mashariki, akapanda meli kwenda Zanzibar (bandari ya pekee ya Afrika ya Mashariki iliyokuwa na mawasiliano kwa meli ya mara kwa mara), akavuka bahari akaanza barani kutafuta machifu waliokuwa tayari kumpa sahihi kwenye mikataba ya kuanzisha uhusiano na kampuni yake. Katika safari ya wiki chache alipata machifu kadhaa waliofurahi kumpata msaidizi wa nje ambaye labda angewasiadia kujikinga dhidi ya Sultani wa Zanzibar (aliyejaribu kuwalazimisha kukubali ukuu wake). Walidhani urafiki na Mzungu wa mbali ungekuwa afadhali, hawakujali iliandikwa nini kwenye karatasi zilizoandikwa kwa Kijerumani.
Mikataba hii ya 1884 ilikuwa msingi kwa kuanzishwa kwa koloni ya Kijerumani na hivyo msingi kwa kuanzishwa kwa Tanganyika.

Huyu Peters kweli alikuwa mtu mwenye tabia baya; alikuwa mbaguzi wa rangi, alidharau watu weusi, alitafuta faida yake tu. Aliamini nia kuu ya kuelewana na wenyeji ilikuwa kuchapa kiboko. Ingawa aliwadharau watu weusi, alikuwa na mpenzi, binti wa Uchaggani, alipomkuta pamoja na mtumishi Mwafrika aliamuru kuwanyonga wote wawili. Hapa serikali ya Ujerumani ilipokea malalamiko kutoka Wamisionari akafukuzwa katika utumishi.
Bila huyu Peters koloni ya Kijerumani isingeanzishwa; hakuna dalili maeneo ya Tanganyika yangekuwa eneo la pamoja bila yeye.
Vipi: Huyu ni baba wa Taifa halisi? Hata kama ni baba kwa njia ya kubaka tu tu?
 
Tafiti zaidi zinaitajika, Pili kuna umuhimu wa kuiweka historia ya nchi yetu pamoja na dunia katika usawa.

Itasaidia kuweka wazi mambo ya kihistoria, na ili kufanikisha hili hatuna budi kukwepa urangi(race), udini na upendeleo wowote ule wenye kutaka kupotosha hali halisi iliyokuwapo kipindi cha nyuma.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…