Karma is real

Nashengena

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
2,913
Reaction score
5,318
Habari za mchana. Yaani jana nimeamini malipo na hapahapa duniani. Kuna rafiki yangu aliwahi kuja na kuishi kwangu mwaka 2018 sababu alikuwa na matatizo.

Alikaa kama mwezi, wakati wa kuondoka akaniomba kiasi cha pesa kama 500k akiahidi atanirudishia. Maisha yakaendelea. Akapata bingo maisha yake yakawa maazuri hadi akanunua usafiri etc. Kuna kipindi nikawa nauguza mama yangu nikamkumbushia ile hela, alinizungusha wee mwishowe maneno ya kejeli. Mimi nikaachana naye.

Yaani jana nikapigiwa na simu ngeni, kusikia sauti nikamuuliza kulikoni umzpotea njia. Ohh naomba tuonane. Kaja jioni karibu na nyumbani, kachoka kwelina hana usafiri. Ananihadidhia kilichompata, eti katapaliwa na rafiki yake wa karibu na anaomba nimkopeshe nauli arudi kwao. Ninamuambia sina apambane na hali yake.
 
Ni kawaida marafik zetu waliopata kaz kukengeuka na kutafuta marafik wapya au kubadili behaviour....juz kuna rafk kaniomba 20k huyu jamaa alipata kaz zur na hakuwahi kunitafuta kaz imeisha amenitafuta jana ANYWAY NMEMPA HIYO 20K
 
Duu. Pole yake.watu hawajui kuwa maisha ni mzunguko
 
Ulifanya vizuri, mtu kama huyo hawezi kuwa na akili ya kuchanganua mambo kama ataendelea kupata msaada mahali ambapo aliharibu. Jinsi atalavyopata stress ndio atajuwa umuhimu wa kuwa muaminifa.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Ni kawaida marafik zetu waliopata kaz kukengeuka na kutafuta marafik wapya au kubadili behaviour....juz kuna rafk kaniomba 20k huyu jamaa alipata kaz zur na hakuwahi kunitafuta kaz imeisha amenitafuta jana ANYWAY NMEMPA HIYO 20K
Ni jambo linauma ila mimi nimejifunza kuwaelewa watu. Mara nyingi watu huwa karibu kwa sababu ya jambo fulani.
Kuna jamaa yetu fulani sasa hivi ni naibu waziri aliteuliwa na magu, wana wanalalamika siku hizi hapokei simu zao sijui anaringa.
Ila mimi namwelewa kwa sababu amepanda ngazi sasa hana cha kuongea nao. Sasa hivi simu zake za mawaziri na watu wengine hakuna connection hapo.
Yale yale ya Hashim Thabiti wana kulalamika haji kijiweni akiwa TZ, jamaa walikuwa wanasahau anacheza NBA si Hashimu yule wa zamani.
Maisha yakipanda na wewe unabadilika. Kuna wale wanabaki hivyo hivyo ila kama mtu akibadilika mwelewe tu ila la msingi akifulia sio anakuja tena kwako maana hapo sasa itakuwa kakugeuza wewe ni rafiki wakati wa majanga.
 
Kama pesa unayo mpatie tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…