Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Kwa ufupi tu,
Kuna wasemaji na wahamasishaji wengi wa Vilabu vya michezo hapa Nchini kuanzia Masau Bwire, Bumbuli, Nuggaz, na wengineo. Hawa wana jukumu kubwa la kuhamasisha mashabiki, kujenga mahusiano na klabu zingine, kujenga mahusiano jamii ya habari na taaasisi zingine nje ya mpira. Pia wana jukumu la kuhakikisha klabu inaungwa mkono na sehemu kubwa ya jamii.
Kiuhalisia hilo suala linafikiwa kutokana na ubora wa hii idara. Tuliona hapo nyuma hamasa kubwa sana ilitokea kati ya Jerry Murro na Hajji Manara , kukawa na utani wa jadi na vijembe mbalimbali lakini all in all kulikuwa na hamasa kwelikweli kwenye soka. Alipoondoka Murro alibaki Manara peke yake kama alama ya usemaji na uhamasishaji wa soka Tanzania.
WHAT WENT WRONG:
Namuangalia Bumbuli halafu namuangalia Nuggaz nikimaliza na Bwire. Nakuja kufanya comparison na HAJJI MANARA, hapa napata walakini. Manara anapenda sana soka na ana ushawishi mkubwa sana uliojengwa kwa mgongo wa Klabu yake Simba Sc. Kuna wakati wa kufanya maskhara na unazi (Mfano Slogan ya Utopo, Vyura, n.k) lakini linapokuja jambo la Serious Hajji alijisahau sana na kulewa sifa hata kuwadharau ambao si Mahasimu zake. Hili ni Mfano tu pale alipomshambulia vkali mwanahabari mwenzake ambaye ni manyakazi wa Clouds kwenye Live interview. Pale hapakuwa na unazi lakin Hajji aliingiza Unazi na alikuwa mkali sana (Out of proffessionalism) na hata walimkanya kuwa yupo Live lakini alionekana kutojali kwa majibu na dharau. Wanahabari walitoa tamko kulaani.
Hii ishu ya Prica wa Clouds ilimkera sana Babra; Manara alipaswa kujua ile ni Press conferemce ya Klabu na waandishi, yeye alikuwa pale kama afisa habari wa timu. Alichokifanya sijui mambo ya wassap message na kufokeana ilikuwa ni "personal issues". Manara jakuwa sahihi kumwambia Mwandishi aliyeuliza swali kuwa "tena wewe ndo unyamaze kabisa... " . Relation kati ya Media na Simba ilikuwa inaharibika kwa sababu za utoto wa Hajji. Babra ameliona hili pia.
Wkati wanalaunch mpango wa Visit Tanzania, Ule ule mpango mzur sana ambao vilabu vingine vilipaswa kuigwa. Hajji kama afisa Muhamsishaji alipaswa kuipiga promo ili iungwe mkono na Vilabu vingine. Lakini Instead kwenye Press kabisa na kwa jambo ambalo ni serious alikuja na Slogan ya "Visit Kidimbwi" kuwa Yanga ndo wanastahili. Matokeo ni kuwa baada ya Yanga kuiga na kuipromo pia ikawa wamejitenga kwa kuonekana ni ya Serikali na Simba. Sidhani kama ile lilikuwa Lengo la kina MO na Babra au uongozi kwa ujumla. Lengo lilikuwa ni kampeni ambayo ingeukwa mkono na taifa zima lakini Hajji bila kutumia akili aliikwamisha na kuifanya ya kinazi.
Wengi walimuacha na Simba kama mashabiki walimshangilia kinazi. Leo hii dharau zake amezipeleka mpaka kwa waajiri wake ambao kwa pamoja wameamua kumkataa. Platform ya Simba sc na mashabiki kwa asilimia kubwa wanamkataa sasa Hajji anakimbilia kwenye Media kulalamika. Media ambayo alishaharibu na walishamlaani kwa matendo ambovu ya dharau. Nani wa kumsaidia. Nuggaz anawatania sana Simba lakini sidhani kama alikuwa anawasemea hovyo sana kwa misingi ya kuleta chuki. Leo Yanga S.c nao wanamcheka Manara.
NANI WA KUMSEMEA? GSM? AZAM? ASAS?
Hawa wamemfuata Manara akiwa juu, anasikilizwa na kujulikana kila Mahali lakini akiwa kwenye platform ya Simba SC. Kiburi kinachomtoa Manara toka Simba kitamfanya asiweze kushiriki jambo lolote linalohusu klabu sababu ya kuwekeana chuki. Ataporomoka Umaarufu. Nani atamuhitaji? Si GSM, SI AZAM WALA SI ASAS.
Manara atulie, Media zinataka kumtangaza akiwa amechuja wamcheke (KARMA law). Manara anapaswa au alipaswa ang`atuke Simba kwa kujiuzulu au angesubiri uongozi umuhoji kwa tuhuma zake kuliko kuropokaropoka mitandaoni ambako anajua ana uadui nako. Nani kamsikia Babra akiropoka?
MANARA ANGETOKA KWA STAHA ANGEENDELEA KUENJOY PLATFORM YA SIMBA NA KUENDELEA KUFANYA DILI ZAKE. AJIFUNZE KWA JERRY MURO AMBAYE HATA LEO YANGA ANAWEZA KUJA KUHAMASISHA JAMBO FULANI NA AKAPOKELEWA NA KUFANYA HATA INTERVIEW.
Nilipokosea nakubali kurekebishwa.
Kazi na iendelee!