Karne ya 21, mwaka 2025, Afisa wa elimu Morogoro hataki matumizi ya computer?

Karne ya 21, mwaka 2025, Afisa wa elimu Morogoro hataki matumizi ya computer?

CHIEFMANGU

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2016
Posts
528
Reaction score
800
Nimeshangazwa sana na aina ya viongozi wa elimu mkoa wa Morogoro, nimemtembelea rafiki yangu morogoro mjini,nimekuta yupo busy kuandika mikaratasi mikuuubwa ya mpango kazi wake wa mwaka.

Namfahamu kuwa ni mtu wa kucheza na computer sanaaa, nimemuuliza inakuwaje unaandika kwa mikono, unachora kwa rula, wakati una computer na unajua kutumia? Jibu alilonipa ndo limenifanya nichokee!

Eti Afisa elimu mkoa wa Morogoro hataki watu waandae nyaraka zao kwa kutumia computer! ANATAKA WAANDIKE KWA MIKONO! Hili limenishangaza sanaaaa, yaani karne hii watu wanalazika kuandaa maazimio ya masomo Yao kwa kuandika kwa mikono??? Sasa mbona walipewa tablets nchi nzima ili ziwasaidie kurahisisha mambo,inakuwaje wanaozitumia wanafokewa, na kutakiwa kuandika kwa mikono?

Je, hii inadhihirisha ujinga wa walimu (maana hata Afisa elimu ni mwalimu) aliousema Tundu Lissu?

Nilitarajia wenginwangekuwa wakihamasishwa kutumia tehama kwenye mambo mengi ikiwemo kuandaa nyaraka za kufundishia, ili walau miaka ijayo watu watumie emails kutuma na kupokea nyaraka mbalimbali za kiofisi, ili kupunguza matumizi ya karatasi, na hatimaye kupunguza ukatili dhdi ya miti!

Tunadhibiti matumizi ya mikaa kupunguza uharibifu wa misitu, lakini upande was pili baadhi ya maafisa wa serikali wanachangia uharibifu wa misitu
Kwa kuongeza matumizi ya karatasi!

AFISA ELIMU MKOA WA MOROGORO change the move, kubali teknolojia inakua na inarahisisha kazi, tuitumie kuhimiza maendeleo ya taifa letu.
jamiiforum
 
Umeamua kukashifu walimu ili kuridhisha nafsi Yako sijashangaa sana maana ni sehemu ya magonjwa ya akili
Juzi nilipata mkaguzi kutoka taifa na nikatumia simu kumuonesha kazi zangu na alipokea kwa furaha huku akipongeza matumizi ya tehama kazini
So sio wote wenye mtazamo kama huo wa afisa elimu wako
 
Soka-mkashfu mtu mbona, otherwise haujaelewa andiko langu, tuliza brain usome tena!
 
Back
Top Bottom