Wakuu wanaJF na wadau wote. Chuo kikuu cha Dar es Salaam kimepitia upya ada zake za masomo ya uzamili na uzamivu ambazo zinatumika kuanzia mwaka huu (2013/2014) wa masomo. Jambo la kushangaza ni kuwa karo hizo zimepanda kwa karibu au zaidi ya asilimia 100% kwa kweli nashindwa kuelewa kigezo au vigezo hasa vilivyozingatiwa ili kupandisha karo kwa viwango hivi?
Kwa mfano, mimi mwenyewe nimemaliza Postgraduate diploma in education (PGDE) hapo mlimani mwaka huu na sasa nipo nafanya teaching practice ili kukamilisha course mbili zilizobaki. Yaani CT513 na FE599. Karo ya course hii ilikuwa 1,647,500/= lakini imepandishwa na kuwa 3,250,000/=; kozi nyingine nazo mwelekeo ni huohuo. Nyingine ni admission fee ambayo ilikuwa 20,000/= lakini imepandishwa mpaka 50,000/= zaidi ya 100%. Kwa taarifa zaidi fungua attachment au fuata link hii: http://postgraduate.udsm.ac.tz/medi...aduate_Studies_Fee_Structure_Revised_2013.pdf
Wadau kwa kweli mpaka sasa nashindwa kuelewa kabisa walizingatia nini hasa? Au ndiyo suala la wasomi na viongozi wetu kuwa out of touch na wananchi? Hebu tulijadili hili suala kwa makini.
Naomba kuwasilisha.