Chungurumbira
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,170
- 571
Sikiri mimi masikini, uvivu wangu nyumbani
Ukiwa huu njiani, nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba, chakula kingi kwa baba
..............................................................malizieni mnaojua
Je, na hivi vitabu vinaweza patikana wapi? Hakuna anayeweza kuscan vitabu hivi?
Ngoja nikuimbie kidogo
1.Sungura afahamikaa ujanja kujijazia
Wenzake wanamcheka sungura huwazomea
Ila siku ikafika ya sungura kuumia
Ya sungura kuumia sungura nakuambia!
2.Siku hiyo akaenda shambani kutembelea
Akayaona matunda mgombani yamejaa
Sungura aliyapenda mgombani kasogea
Mgombani kasogea sungura nakuambia
3.Sungura karukaruka lakini hakufikia
Matunda hakuyashika mkononi kuyatia
Hakika alisumbuka nguvuze zikapungua
Nguvuze zikapungua sungura nakuambia
4.Yakamtoka machozi matunda akalilia
Matunda akalilia sungura nakuambia
Sizitaki mbichi hizi sungura kajisemea
Naona nafanya kazi bila faida kujua!
hivyo yani Kama nimekosea nirekebisheni
Ngoja nikuimbie kidogo
1.Sungura afahamikaa ujanja kujijazia
Wenzake wanamcheka sungura huwazomea
Ila siku ikafika ya sungura kuumia
Ya sungura kuumia sungura nakuambia!
NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:
1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.
2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.
3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?
4.Baba aliye kufani akajibu lile swali
Ninakufa maskini baba yenu sina hali
Neno moja lishikeni kama mnataka mali
Kama mnataka mali mtayapata shambani
5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?
6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.
7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.
8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili.
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili.
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali.
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali.
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali.
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
11. Wakanunua na ngombe, majike kwa mafahali.
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli.
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali.
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali.
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli.
KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI.
Mtunzi... x,y
sadiki mimi askini uvivu wangu nyumbani
nakufa hapanjiani daaah nimesahau
Itakua vizuri sana ukiweka na lyrics za ile shairi la "majira yetu haya yangekuaje sasa,utumwa wa nchi..."
NI mojawapo ya mashairi ambayo wengi waliosoma shule za msingi za umma za Tanzania watakuwa wanalikumbuka; lilianza hivi:
1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.
2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.
3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?
4.Baba aliye kufani akajibu lile swali
Ninakufa maskini baba yenu sina hali
Neno moja lishikeni kama mnataka mali
Kama mnataka mali mtayapata shambani
5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?
6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.
7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.
8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili.
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili.
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali.
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali.
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali.
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali.
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani
11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali.
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli.
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali.
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.
12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali.
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali.
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli.
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".
Mtunzi... x,y