Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 775
- 1,332
Timu ya taifa ya Zanzibar ‘Karume Boys’ imeondolewa katika mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, yanayoendelea kutimua vumbi Burundi kutokana kuchezesha wachezaji 12 waliozidi umri.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye, kwa wandishi wa habari, Zanzibar imetimuliwa katika mashindano hayo kutoka na kukiuka kanuni za mashindano.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, kosa la Zanzibar ni kuchezesha vijeba 12 kinyume sheria za uendeshaji wa mashindano hayo, kanuni namba nne, kifungu cha 4.3 na 4.6 na kutokana na kosa hilo, kamati ya maandalizi kwa pamoja ilikubaliana Zanzibar inastahili kutumikia adhabu tatu.
Musonye aliainisha adhabu hiyo ya Zanzibar kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni zinazotakiwa kulipwa na Shirikisho la Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi.
Aidha, kwa kosa hilo, Zanzibar wamefungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.
“Kwa mujibu wa kanuni zetu, Zanzibar wamekutwa na hatia na hivyo, kwa kosa la kuchezesha wachezaji wenye umri mkubwa kamati ya mashindano imeamua kuwaondoa mashindanoni kuanzia sasa”, Ilisema taarifa hiyo na kuendelea.
“Aidha watalipa faini ya dola 15,000, pesa hizi zitarudishwa kwa wadhamini wa mashindano haya ambao ni shirikisho la soka duniani (FIFA), Zanzibar hawataruhusiwa kushiriki mashindano yote ya Cecafa mpaka pale watakapolipa faini.”
Wakati huohuo, wachezaji watatu wa timu ya taifa ya Ethiopia, wamekumbana na rungu la CECAFA kutokana na kukutwa na kosa kama la Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa ya Cecafa, wachezaji hao wamefukuzwa kwenye mashindano hayo kutokana na kuwa na umri mkubwa zaidi ya umri unaokubalika kikanuni.
Kutokana na kosa hilo, Ethiopia wamepokonywa ushindi wa 3-0 walioupata katika mchezo wa kundi B dhidi ya Somalia.
Aidha, Shirikisho la soka la Ethiopia wamepigwa faini ya dola 5,000, pamoja na kutoruhusiwa kujaza pengo la wachezaji hao.
Chanzo: Mwanaspoti