'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'- Karume Jnr

Karume hakukimbia mapinduzi kwani alikua hajui kinacho endelea...mambo yalipangwa Tanganyika na watanganyika kuondoa uislam znz.
Karume akapewa na sera ya mwanzo ilikua kuwadhalilisha masheikh wakubwa ....hakuna cha kujivunia hapa
 
Karume hakukimbia mapinduzi kwani alikua hajui kinacho endelea...mambo yalipangwa Tanganyika na watanganyika kuondoa uislam znz.
Karume akapewa na sera ya mwanzo ilikua kuwadhalilisha masheikh wakubwa ....hakuna cha kujivunia hapa
Kumbe lengo la yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964, ilikuwa ni kupindua dola la Kiislamu la Sultani na kuweka dola ya Kikisto ya Juliasi?!. Kwa vile mapinduzi yale yalifanikiwa sana ndio maana hadi kesho tunaimba mapinduzi daima, hiyo dola ya Kikristo ndio hii inayotawala Zanzibar?!, na ndio inayomnyima Maalim ushindi?!. Baada ya kufanikiwa kuuondoa Uislamu Zanzibar, kumbe sasa Zanzibar ni taifa la Kikisto!.

Mapinduzi Daima!.

Pasco
 
Maalim Seif alikua vizuri kukaa kimya kuliko lile tangazo alilotoa Mansur Yusuf Himid la kususia sherehe za Mapinduzi matukufu, hii inawapa washindani wake nafasi nzuri ya kumsema kwamba hapendi Muungano na anapinga uwepo wa Baraza la Mapinduzi.

Hata Tangazo lake la jana bado halijampa nafuu ktk siasa amechelewa sana watu wako mashambani.
 
Nawatakia kumbukumbu njema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyovikomboa visiwa hivi.
P
 
Tuulize sisi tuliokuwepo Zanzibar, wchana na vijarida vya kubuni story chonganishi.Mzee Thabiti Kombo amelibainisha hilo.
Je wewe na Thabit nani mkweli>?
 
Ahsanta mkuu nimekusoma kwa utuvu.
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Wewe si ni Mjukuu wa Masulutani, tuachie tufurahie siye
 

Hivi nawewe huna Babu yako aliyekimbilia Zanzibar kama Magufuli?
 
Okello alikuwa polisi hapo Zanzibar ingawa alikuwa ametokea Uganda.
Sidhani kama Okello alikuwa ndani ya jeshi la polisi kama mtumishi. Kumbuka Okello hata kiswahili kikimsumbua, fuatiliza video za mahojiano kwenye youtube. Lugha ikimsumbua ya kiswahili, huu kwangu ni ushahidi alihamia Zanzibar si zaidi ya miaka michache kutokea Uganda kuelekea Mapinduzi.

Lengo kudadisi waliopanga Mapinduzi sio kuyahalalisha, bali kuondoa upotofu uliopo kuwa mapinduzi yalimwondoa Sultan wakati ukweli iliondolewa serekali halali kwa sheria na taratibu za wakati huo. This is just a fact, hata kama hupendi monarchi style zipo nchi nyingi tuu duniani na nyengine afrika zina wafalme.
 
Just googling Okello alihamia muda gani visiwani Zanzibar, alihamia miaka 4 kabla ya Mapinduzi.
John Okello, a Langi from the present-day Alebtong District in northern Uganda. He had gone to the island four years earlier.
REF:
 
Watu wenye akili za kufikiria nje ya box, Okello hakuhamia as coincidence. He was a men in a mission, a retired military trained in Cuba. Wengine watasema ni speculation kama alifundishwa uharamia kwa Castro. Kwangu siamini bahati mbaya, naconnect dots hadi kwa Julius.
 
Alikuwa polisi mzee wangu; kuna rekodi nyingi zinathibitisha hivyo. Alikuwa ni polisi aliyeachwa na wakoloni hakuwa wa mapinduzi. Wakati huo waingereza walikuwa wanatawala Kenya, Uganda na Tanganyika na Zanzibar, kwa hiyo kwao wao askari atokee Kenya au Uganda lilikuwa jambo la kawaida sana. Hata idi Amini aliwahi kutumika kwenye jeshi ta KAR kambi ya Tabora
 

Okello hakuwahi kuwa polisi Zanzibar, Yawezekana wewe unamchanganya na Edison Kisasi
 
Utaishi vipi polisi Zanzibar halafu usijue kiswahili ? Kwa kiswahili cha Okello, miaka minne nadhani ni very conservative estimate. It should be much lower than that!
 
Utaishi vipi polisi Zanzibar halafu usijue kiswahili ? Kwa kiswahili cha Okello, miaka minne nadhani ni very conservative estimate. It should be much lower than that!
Siyo kuwa kila aaliyekuwa akiishi Zanzibar alikuwa anajua kiswahili. Okelo alikwenda kwanza Kenya kutafuta kazi, akapata kazi ya hovyo hovyo kwa vile hakuwa na elemu, aliposikia zanzibar kuna kazi za upolisi ndipo akaenda kujaribu na akafanikiwa. Kujua lugha huwa inategemea na kichwa cha mtu, wengine ni wazito na wengine ni wepesi. Tuliwahi kusimuliwa hadithi yote ya mapinduzi yale na Brigedia Yusufu Himid pamoja Kanali Abdallah Natepe mwaka 1976; wao wamo kwenye picha hii pamoja na Okello.



Kimoja walichosema wote ni kuwa kwa vile Okello alikuwa haogopi kitu na alikuwa na lugha ya kutisha na sauti ya ukali sana kwa kutumia amri za kipolisi, ndiye aliyekuwa mbele ya mapinduzi yale na aliwatia hofu sana watu wa serikali. In fact alipovamia kituo cha polisi kupora silaha ni kwa vile alikuwa anafanyia kituo hicho hicho na alikuwa anajua silaha ziko wapi.

Ndani ya picha hiyo unaweza kuwaona Abdallah Natepe na nyuma ya Okello, na Yusuf Himid pembeni mwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…