Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Tanzania tuna Virume kadhaa, tuna Karume mwasisi wa Muungano, Karume Rais wa mwisho mstaafu wa Zanzibar na Karume balozi mstaafu. Kwa vile Karume mwasisi alishatangulia mbele ya haki, hatuwezi kujua leo angesemaje kuhusu huu Muungano, bali alikuwa ni mwasisi na mtetezi mkubwa sana wa muungano huo kabla hajakumbwa na mauti. Swali langu linahusu hawa Virume wawili tulio nao kwani wamekuwa wakitoa kauli zinazokinzana sana kuhusu Muungano huu. Mmoja anataka mfumo wa Muungano uliopo uendelee ila ufanyiwe marekebsiaho madogo madogo wakati huyu mwingine akitaka muungano ufumuliwe kwa kina sana kiasi cha ama kuwepo ama kwa serikali tatu au ikiwezakana kabisa basi hata Zanzibar ijitoe katika Muungano huo.
Kati ya Virume hawa wawili, nani yuko sahihi? na ni kwa nini undahani yuko sahishi?
Kati ya Virume hawa wawili, nani yuko sahihi? na ni kwa nini undahani yuko sahishi?