Wakuu,
Inabidi tuwe tunafanza utafiti na kile tunachoandika kwani bila hivo basi kila kile tuandikacho kitakuwa kimekosa mwelekeo.
Ni wazi kabisa kwamba wenzangu wote tunaondika hapa kuhusu hayati Karume ama tunafanza makusudi kupotosha au bado tunakuwa hatufahamu kwa undani historia ya Zanzibar na matukio yaliyotokea kisiwani humo kabla na baada ya mapinduzi.
Lakini si taabu kwani ni vizuri kuwa na mjadala ambao labda baadae unaweza kutoa mwanga juu ya nini hasa mzee huyu alikifanza kabla na baada ya mapinduzi.
Zanziba kilikuwa ni kituo cha biashara ya utumwa na inajulikana wazi kwamba baada ya waarabu kutawala mahala pale mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, mwishowe walikuwa wanazaa na waafrika.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba baada ya zahama na shida kubwa ya waafrika kuwa manamba na vibarua katika mashamba ya karafuu na kwamba hata baada ya mapinduzi waarabu kuonekana bado wameneemeka kwa majumba ardhi na fwedha, hayati Karume (kwa akili yake) aliona jambo hilo na kwa mtazamo wake akaona kwamba ni lazima pawe na usawa kwa kila kitu na hapo ndio mzozo ulipoanza.
Kwa hio kwa hatua hizo nzito za kuua watu, kufanza watu wapotee kusikojulikana, kulazimisha ndoa za waarabu na waafrika na kuwaandama wale ambao hawakuona kwamba mambo hayo yanastahiki kufanzwa, naona kwamba nnaweza kusema kwamba tuhuma zinazotolewa ni sahihi.