mimi sasa nashawishika kwamba huenda sera ya mwalimu ya usawa,ujamaa na kujitegemea huifahamu vizuri, mwalimu alikuwa anaamini hivi "Binadamu wote ni ndugu zangu na afrika ni moja"
Kwa hio unamaanisha kwamba kama binadamu wote ni ndugu? Mbona kama ni hivo basi hata wale ambao ni MAFISADI kwa sababu ni ndugu basi tuendelee kuwachagua na wale maskini wa kutupwa waendelee kula mlo mmoja kwa siku na kutembeza godoro toka tandika mpaka Kariakoo na asipate mnunuzi huku wengine wakifaidi matunda ya uraia wa Tanzania?
alikuwa tayari kupambana na Fisadi mweusi(mfano nduli Amini) na pia kupambana na fisadi mweupe(mfano kaburu) au rangi yoyote ile. na alikuwa tayari kuwa rafiki na yeyote yule ambaye ana misingi ya utu. sasa ndugu yangu unashangaa kweli mwalimu kufia ulaya?,
Hii yote ni siasa ndugu yangu. hayati Mwalimu alikuwa ni miongoni wa "elites" watu wenye uswahiba na mabepari lakini kwa mtindo wa aina yake ambapo mtu asiekuwamo humo hawezi kuelewa.
Ukisoma kuhusu vita baridi iliyoanza mwishoni mwa miaka ya sitini mpaka mwanzoni mwa miaka ya themanini na kuilewa yote ndio utajua kuwa Afrika hatuna watu ambao wewe tunawaita ndugu na kwamba eti Afrika ni moja.
Je unajua ni sababu zipi hasa zilimfanza Idi Amin amchokoze hayati Mwalimu? na ni nani walimsaidia Amin kuwa kiongozi wa Uganda? Nenda kasome tena na uchambue historia halafu utaniambia.
Afrika sio moja kwa kuangalia mifano ya nchi kama za Botswana, Namibia, Mozambique zenye kuonesha kwamba zina uwezo wa kuajiri na kuwajali madaktari wa Tanzania.
Lakini tutaendelea kuwa wajinga kwa kuendelea kufikiri kwamba viongozi tunaowachagua ni wale wenye nia njema za kuendeleza jamii ya watanzania kwa kuhakikisha tunafanza hata nusu ya hawa waliotangulia kimaendeleo kwa kuwa na hata hospitali moja yenye specialists wa kila ugonjwa na vifaa vya kisasa kama X-Rays, UltraScans na vingine.
Kwa mfano Ultrascan inasaidia kujua ni sehemu gani katika mwili pana uvimbe au damu imevia kwa muda mfupi mno,na mengine ambapo ndio unaambiwa eti mzee kaenda kuangaliwa afya yake.
Sasa kama hatuwezi kuwa na Ultrascan za kutosha katika nchi yetu ndio hivo tena tunabaki tukishangaa watu kwenda majuu kwa uchunguzi wa kiafya.
Kwa hio nahitimisha kwa kusema kwamba kitendo cha "elites" wa Tanzania kwenda Ulaya kwa matibabu na kutumia "change" inayobaki kupeleka baadhi ya wagonjwa nchini India na kwingineko kwenye bei nafuu, sio kibaya kwani hatuna "specialists" wa magonjwa hayo.