Karume1+karume2+karume3=ufalme?

Katika viongozi wote TZ ni Ali Karume pekee alietamka kuwa, iwapo atachaguliwa kuwa Prez Zanzibar ataanzisha serikali ya Mseto. Alisema hayo hata kabla ya Makubaliano ya Muafaka kuwekwa hadharani.

Unazi unawazidi sasa hii ni sera ya CUF hata Balozi Ali hajatamka hayo au kwa msemo wako Kiongozi wa Tz ni anayetoka CCM tu na tunavyowajua CCM tamko la mtu mmoja halisaidii kitu tumeyaona yalotokea Butiama, Mwenyekiti wao alijipiga kifua mbele kuwa atamaliza mzozo wa Znz kazidiwa hoja na Karume sasa ameuzidisha kuwamgogoro zaidi.
 
Kwa maneno mengine hata muafaka wa mwaka huu ni bomu?
 

Hebu soma hapa chini vizuri:
 

Waridi uniwie radhi kwa kukuvurugia topic yako.
Hii ni quote toka kwa Augustine Moshi
"...Mwisho, natoa onyo: Hakuna kitu kibaya zaidi ya inferiority complex. Inafisha jumuiya. Wale ambao mnajisikia inferior, basi leleeni hiyo complex kikwenu, msieneze huo ugonjwa kwa wengine."

Umesema una sababu zako, ...nami nimejaribu kueleza sababu zangu. Please understand that I'm not against you, but the view of ALL who misuse the use of those two terms.

Nisingependa mjadala ubadilike, mwenye interest na issue ya NDIVYO TULIVYO aende kwenye thread hii nilokwisha itaja. Zipo nyingine pia, tumia search.
 
Kwa maneno mengine hata muafaka wa mwaka huu ni bomu?

T'aabaan. Muafaka kama ungelikuwa kama walivyotaka CUF (Mh. Seif) bila ya shaka ungekuwa ni BOMU. Kwani ungekuwa muafaka wa kuleta rehma kwa kundi la wachache (viongozi- pengine wa pande zote), lakini sio wa faida kwa wananchi ambao ndio waathirika wakuu wa hali ya hivi sasa. CCM ilichofanya ni kuuokoa muafaka huo (kwa yale mapendekezomya maerekebisho) ili kuurejesha katika njia ya faida kwa wananchi wote badala ya ku-focus kwa viongozi tu na hatma zao, na ndio maana ikataka hatimaye wananchi washirikishwe kwa ukamilifu katika kuamua mustakabali.
 
Hebu soma hapa chini vizuri:

Hii habari unayoinakili ni mahojiano yalofanyika baada ya Balozi Karume kuondoshwa ubalozini Ujerumani akisubiri kupangiwa kazi na Bosi wake Kikwete - mimi niliyaoma mahojiano yote hayo.Kutumia recently citation kutaka kupindisha ukweli haisaidii.
CUF walisema wataunda serikali ya Umoja tokeo wakati wa Kampeni za Uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…