Kaseja aachwa rasmi yanga

Kaseja aachwa rasmi yanga

Salamander

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
28,536
Reaction score
15,746
1978850_1124198354261248_1488902075069425870_n.jpg

Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na Golikipa wake Juma Kaseja kuanzia leo baada ya kuwepo kwa hali ya kutoelewana baina ya kipa huyo na uongozi wa klabu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa Juma Kaseja alivunja masharti ya mkataba huo kwa kutohudhuria mazoezini na kuongeza kuwa Jumamwenyewe alishaonesha nia ya kuondoka klabuni hapo hivyo ni bora klabu hiyo ikamuachia.

Muro amesema “Yanga haijavunja mkataba na Kaseja bali imemuachia baada ya Kaseja mwenyewe kuvunja masharti ya mkataba kati yake na Yanga...”

Baada ya kuachwa Yanga, unafikiri Kaseja atakwenda timu gani?

Habari imetoka:
East Africa Television (EATV)

Mimi ninawaza tu: Kwanini hawakumuacha December 2014 kabla usajili wa dirisha dogo kufungwa ? Au hawajui soka ndio kibarua chake!
 
atacheza kokobichi fc wao wanasajili kila siku
 
Hata watu wake Simba hawamtaki. Ilikuwa makosa kumsajili toka mwanzo. Lakini kesha vuna sana
 
kama alijua soka ni kazi yake kwanini atege kazi.
1978850_1124198354261248_1488902075069425870_n.jpg

Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na Golikipa wake Juma Kaseja kuanzia leo baada ya kuwepo kwa hali ya kutoelewana baina ya kipa huyo na uongozi wa klabu.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa Juma Kaseja alivunja masharti ya mkataba huo kwa kutohudhuria mazoezini na kuongeza kuwa Jumamwenyewe alishaonesha nia ya kuondoka klabuni hapo hivyo ni bora klabu hiyo ikamuachia.

Muro amesema "Yanga haijavunja mkataba na Kaseja bali imemuachia baada ya Kaseja mwenyewe kuvunja masharti ya mkataba kati yake na Yanga..."

Baada ya kuachwa Yanga, unafikiri Kaseja atakwenda timu gani?

Habari imetoka:
East Africa Television (EATV)

Mimi ninawaza tu: Kwanini hawakumuacha December 2014 kabla usajili wa dirisha dogo kufungwa ? Au hawajui soka ndio kibarua chake!
 
kama alijua soka ni kazi yake kwanini atege kazi.

Kama ukisoma vizuri hiyo habari utaona kuwa kulikuwa kutoelewana kati ya Kaseja na uongozi wa Yanga, na hapa tumeona maelezo ya upande mmoja tu, tusubiri maneno ya Kaseja pia kabla ya kuhukumu. Soka la Bongo limejaa majungu na kukomoana. Kwa mtazamo wangu maamuzi haya yangefanywa kwenye kipindi muafaka ili akatafute ugali kwingine.
 
ila Jerry muro nae hii habari kaitoa kinafki sana, jamaa keshasahau majanga yalomkuta kwa sababu ya ujivuni wake, eti anadai kaseja kamwaga mboga wao yanga wanamwaga ugali. Muro asipokuwa makini atajifuta mwenyewe kwenye tasnia ya habari, kutoka TBC hadi yanga bado anajiona yupo juu, katolewa kwa aibu maximo, ngoja nae Manji amchoke, jamaa sijui kwa nini anapenda sifa laini,.
 
Back
Top Bottom